
Hapa juu ni picha niliyopiga Babati, mwaka 2007 au 2008.

Nilikuwa hapo Babati na wanafunzi kutoka chuo cha Colorado, ambao walikuja Tanzania kwenye kozi niliyotunga kuhusu mwandishi Hemingway. Katika picha naonekana nikiendesha darasa.

Hapa juu, chini ya dirisha, anaonekana profesa William Davis wa chuo cha Colorado, ambaye alitanguzana na wanafunzi, akanisaidia kufundisha kozi hiyo. Alikuwa hajawahi kuja Afrika, na kwa hivyo alitaka kupata uzoefu.
3 comments:
Nimeipenda kazi yako,hakika huo ni wito wa kujitolea kwa ajili ya kuendeleza vijana wa Taifa letu na ulimwengu huu.Mungu akupe moyo wa huhudumia viumbe wake.Hongera,ulipiga picha miaka ya nyuma lakini leo umefika na wanafunzi wako walione 'live'
Tupo tunafuatilia mtandao wako.endelea hivyo Prf.
Kazi nzuri ndugu,Kila la kheri!!
Post a Comment