Jana nilienda Peramiho, mji ulio karibu na Songea. kwa kweli, Peramiho haifahamiki kama mji. Ni misheni kubwa ya Kanisa Katoliki. Kuna kanisa kubwa, seminari kuu, hospitali, duka la vitabu, na kiwanda cha uchapishaji.
Nimefurahi kuona sehemu kadhaa za Peramiho.Picha nilizopiga nitaziweka katika blogu hii hivi punde, Insh'Allah.
Vile vile, nimepata fursa ya kutembelea chuo kikuu cha Songea, kinachoendeshwa na Kanisa Katoliki. Taarifa nitazileta hivi punde, Insh'Allah.
Saturday, July 21, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
2 comments:
Usichelewe kuleta hizo habari na hizo picha nina usongo kweli wa kuona...
Hatimaye, wiki nyingi baadaye, nimeanza kuzileta hizo picha, kama ulivyoziona hapa
Post a Comment