Saturday, October 31, 2009

KWANZA JAMII limetua Mwanza


Gazeti la KWANZA JAMII linapatikana Mwanza, kwa mujibu wa picha hizi zilizotoka katika blogu ya Mjengwa tarehe 29 Oktoba, 2009 na 30 Oktoba, 2009. Nami napenda kufuatilia maendeleo ya gazeti hili.

4 comments:

Simon Kitururu said...

Polepole ndio mwendo!
So far so good!

Mbele said...

Ndugu Kitururu, shukrani kwa ujumbe wako. Labda niongeze tu jambo linalonihusu mimi mwenyewe. Kazi ya kuandika makala kila wiki kama ninavyofanya ni ngumu, kwa sababu shughuli yangu ya msingi ni ualimu. Makala hizi naandika kama shughuli ya ziada, na si rahisi kupata muda wa kutosha kujiandaa vizuri. Nadhani itakuwa bora wengine nao wajitokeze wawe wanaandika pia

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mimi pia huwa najaribu mara moja moja kupeleka makala lakini kama ulivyosema Prof. ni kazi kweli kweli kwani muda haupo. Wakati huo huo mtu unataka uandike makala inayovutia na yenye mantiki.

Nijuavyo hata hivyo ni kwamba gazeti hili halina shida ya waandishi wa makala. Kinachotakiwa -na Mjengwa anajua - ni kulitangaza vizuri. Gazeti pia lijaribu kutenga kurasa chache kwa ajili ya habari za vijijini. Blogu ya Mjengwa imejipatia umaarufu kwa kuandika na kuleta picha halisi za maisha ya kijijini. Ningependa kuona angalau ukurasa mmoja unatengwa kwa ajili tu ya habari za kijijini.

Gazeti la rai enzi zile na sasa Raia Mwema ni magazeti ambayo yanaheshimika sana kwa watu wanaotaka kusoma makala za uchambuzi wa kina na sioni kwa nini Kwanza Jamii lisifikie mafanikio haya.

Bwana Kitururu - unaonaje ukianza kupeleka baadhi ya post zako kutoka kwenye blogu yako ya kifalsafa katika kakipengele ambako tunaweza kukaita "Kona ya Kufikiri" au "Fikra Pevu". Na kwa vile unazo post nyingi tayari katika blogu yako, hutakuwa na shida ya kuziandaa. Naamini kipengele hicho kitakuwa maarufu kweli kwani post zako nyingi, mbali na kuburudisha zinafikirisha na napenda jinsi ambavyo huwa unaziandika. Zitakubalika. Niseme kama ambavyo huwa unapenda kusema "nawaza tu mkuu!"

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yep. mwezi mmoja uliopita nilipigiwa simu na binti aitwaye Jannet wa Mwanza akitaka kujua zaidi mambo ya utambuzi japo sikuweza kuonana naye nilipoenda manza hiyo kama ishara nzuri ya kusomwa kwa gazeti hilo na kwa hakika utambuzi pia unapendwa sana na wasomaji.

japo Bukoba sijaliona hili gazeti

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...