Wednesday, October 7, 2009

Sea--Papi Kocha, Nguza Viking

4 comments:

John Mwaipopo said...

Prof na wewe umo kwenye mambo hii? ha! ha! ha!

inaonyesha ni kwa jinsi gani ulivyo simple.

Nyakati huja na kuondoka. sauti ya jela.

napapenda "wenye kusemasema oooh Seya wabaki vinywa waziii

Mbele said...

Kama ni kuyaruka majoka tu, mimi ndio mwenyewe, tena sana. We acha tu :-)

Anonymous said...

duh! professor mbele huwa nakukubari sana mambo yako sema wewe ni mtanzania lakini kwa jina tu sidhani kama kuna kitu unakifanya hapa nyumbani zaidi ya ughaibuni,ila poa mungu ndo hupanga maisha ya kila mwanadamu wapi aanzie wapi amalizie,goodluck!

Mbele said...

Anonymous, shukrani kwa ujumbe wako. Kuna mambo mengi sana nafanya hapa Tanzania. Pitia pitia blogu zangu utaona taarifa kem kem.

Ila napenda niseme pia kuwa waTanzania wakati mwingine hawako makini. Kwa mfano, miaka mitatu iliyopita, nilitangaza kuwa naendesha warsha mijini Tanga na Arusha, na matangazo yalitokea kwenye blogu zangu, hata blogu ya Michuzi.

Nilililipa gharama zote za maandalizi, ikiwemo kulipia kumbi na mimi mwenyewe kujilipia gharama za usafiri, malazi na chakula. Hakuna m-Tanzania hata moja aliyekuja.

Tofauti, hapa Marekani mimi sitangazi warsha wala mihadhara, bali wao wanaandaa na kunialika nikazungumze. Wanaheshimu ujuzi wangu.

Ujuzi huo ninauweka pia katika vitabu ambavyo naandika. Nimefanya juhudi yangu mwenyewe kuvileta vitabu hivyo Tanzania. Vinapatikana hapa Dar es Salaam. Lakini wa-Tanzania kwa ujumla hawana habari navyo, kwa maana kwamba hawavitafuti, hata nikiwaambia kuwa vinapatikana na simu namba nikawapa, yaani 0754 888 647 na pia 0717 413 073.

Hivyo hawavihitaji, inavyoonekana. Nina hakika kuwa ningefungua baa wangekuwa wanajaa hapo nami ningepata umaarufu sana.

Kwa ufupi, huo ndio uzoefu wangu, na kama nilivyosema, pita pita kwenye blogu zangu, utaona mengi. Narudia tena kukushukuru kwa kupitia hapa kwenye kibaraza changu, na usisite kupita tena, mara kwa mara, na kutoa mawaidha au kunikosoa, maana elimu haina mwenyewe.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...