Wednesday, October 28, 2009

KWANZA JAMII Mikumi

Picha hii imechapishwa tarehe 28 Oktoba, 2009, katika blogu ya Mjengwa. Maggid Mjengwa amepiga picha hii Mikumi. Mimi kama mwandishi katika gazeti la KWANZA JAMII nafurahi kuona gazeti hili, ambalo bado changa, linavyojikongoja na kuendelea kuenea nchini, hadi kwenye miji midogo na vijijini. Siku chache zilizopita tulipata habari za KWANZA JAMII kufika kijijini Roya. Bofya hapa. Kama wahenga walivyosema, pole pole ya kobe humfikisha mbali.

9 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ajabu na muujiza mkuu ni kwamba gaziti hili halipatikani popote pale katika mji wa Bukoba

Mbele said...

Shukrani kwa hii taarifa. Ni changamoto kwa wahusika, wajitahidi likafike kule. Kama kijijini kwangu kule milimani Umatengo (Mbinga) gazeti hili linafahamika, haikubaliki kwa nini lisitue kwenye jiji hili la akina Rugarabamu na Ndyetabula :-)

John Mwaipopo said...

hapo hapo profesa. hakikisheni mnaongeza ujuzi na maarifa katika tasnia hii ya uandishi. naamini kuwa kwa kuwa wengi wa waandishi wa gazeti hili mu-wanazuoni hodari basi hamchoki kujifunza kila uchao mbinu na ujuzi mpya wa uandishi usisimuao ili muweze kuteka hisia za sie wasomaji.

Mbele said...

Ndugu Mwaipopo, ushauri wako ni mzuri kabisa. Ni wajibu kujitahidi kuboresha shughuli muda wote.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yep na inabidi tulifanye la kisasa na lenye nia ya kuwakomboa watu wetu au sio/

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

prof. najiuliza ni kwanini blog yako ya kiingereza huruhusu kapeku kama mimi kuiembelea eti kuna invitation, kwa nini? ni invite basi namimi au niya kifamilia zaidi?

Mbele said...

Ndugu Kamala, shukrani kwa mawaidha yako. Kuhusu hili la blogu yangu, sikuwa nimetambua kuwa kuna vizuizi. Nitaangalia kulikoni. Mtu asikudanganye, nami ni peku wa masuala ya hizi tekinolojia.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mwaipopo: Njia rahisi ya kulifanya gazeti liweze kuteka hisia za wasomaji ni kuanza kuandika UDAKU!

Uzembe ule ule uliopo katika kusoma vitabu upo pia katika kusoma makala ndefu za uchambuzi wa kina. Watu "hawana muda". Wasomaji wanataka habari fupi fupi zilipambwa kwa picha za wasichana waliovaa "vivazi" na vichwa vya habari vya kuvutia kama "Mwaipopo akutwa akila denda uchochoroni", "Mwaipopo hoi kwa penzi la Mwanaisha". Basi hapo utaona gazeti litakavyonunuliwa. Upo?

John Mwaipopo said...

nzuzulima:-)

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...