Sunday, March 20, 2011

Kazi ya Kunywa

Ukiondoa kazi ya kukaa vijiweni, kazi muhimu ya wa-Tanzania wengi ni kunywa. Huyu jamaa kwenye katuni ni m-Tanzania halisi. Yuko kazini, wala hafanyi mchezo. Ameshaamrisha kuwa kaunta ihamie hapa alipo, tena haraka sana.Wako wa-Tanzania ambao wanajifunza kunywa tangu utotoni. Wanapofikia ujana wanakuwa wameshahitimu.

Kazi ya kunywa ni muhimu kwa wa-Tanzania wengi kiasi kuwa wamehamia baa, na wanaishi huko, kama nilivyoandika hapa.

Shughuli nyingi za jamii Tanzania zinawezekana tu iwapo zinaendana na kunywa. Yaani ili watu waje kwenye hizi shughuli, ni muhimu ulabu uwepo. Hata kwenye uzinduzi wa kitu kama kitabu, ni muhimu pawe na ulabu, kama nilivyoelezea hapa.

Nilisoma kwenye jarida la Tanzania Schools Collection, 1, (2009), kuwa mtoto mmoja wa miaka kumi alionekana kwenye maonesho ya vitabu Dar es Salaam akiwa mwenyewe. Mratibu mojawapo wa maonesho alipomwuliza kwa nini hakuja na baba yake, mtoto alijibu kuwa baba angefika kama kungekuwa na bia (uk. 12).

Kwa mwendo huu, naweza kusema kuwa miaka ijayo, itabidi tuwe na bia kila mahali, kuanzia shuleni hadi Bungeni.

(Katuni nimeipata katika kitabu cha Kula...Mtoto wa Bosi, kilichoandikwa na Simon Regis na kuchapishwa na Regis Art Production, Dar es Salaam. Sikumbuki ni wapi nilipata hii picha nyingine. Ningependa kuweka taarifa ipasavyo)

10 comments:

emu-three said...

Profesa kukiwa na bia kila mahala, nina wasiwasi kuwa hata hicho kitabu kitalowa pombe!....maandishi yatapotea na mwisho wa siku ...inageuka nchi ya walevi!

Katu said...

Nashukuru Profesa Mbele kwa kututanabaisha undani wetu sisi watanzania....

Tanzania inahitaji total reform ya mfumo wa elimu hasa ya shule za msingi na sekondari ili kujenga jamii inayojitambua kwa undani zaidi kuliko sasa.

Tanzania ya leo ni jamii iliyokata tamaa inayoishi bila kujua kesho kuna nini! Na huu ndiyo msingi wa kuangukia kwenye ulevi wa aina zote ngono, unga(madawa), madaraka na vileo(Pombe) pia.

Jamii yetu hivi sasa imejengwa upungufu mkubwa kujibidisha kufikiri na kuwa wabunifu katika masuala muhimu kwa ajili maisha baadae matokeo yake uvivu wa kufikiri hupo kila kona kuanzia mwananchi wa kawaida mpaka viongozi wa juu serikalini.

Na dalili mojawapo na kiasharia tosha ni ulevi wa kupindukia ambao mara nyingi unatokana na uwezo wetu kutafakari mambo na maamuzi muhimu kuwa wa kiwango cha chini sana.

Nchi nyingi zilizoendelea ziliwekeza fedha katika tafiti na tathimini kupata Taifa lenye miradi endelevu.

Leo hii hapa Tanzania Taasisi zenye mamlaka ya kufanya tafiti mbalimbali za miradi maendeleo na kisayansi wanalenga kwenye kuandikia tafiti kutoka kichwani kwao tuu na siyo ukweli halisi..

Ambapo hizi tafiti zingeweza kutumika kuelemisha watanzania madhara na athari ya ulevi katika rika zote zilizopo katika jamii.

Inasikitisha iwapo ukiona viongozi wa juu serikalini wanahimiza jamii katika katika mradi wowote wa maendeleo basi bila shaka ni m-mi-radi yenyekufadhiliwa na mashirka ya nje.

Hivi ni kweli hakuna vitengo vya tafiti katika wizara za serikali na mashirika binafsi!!!?.

Kimsingi Profesa Mbele, suala hili la ulevi hupo katika jamii yetu lakini tukubali kuna tatizo la msingi wataalamu wanaita (R&D=research and development).

Mbele said...

Ndugu emu-three, hali ndio hiyo. Tena naona nchi imeshageuka ya walevi. Hadi vijijini, miaka hii, utawakuta watu wamejaa kilabuni, saa nne asubuhi.

Ndugu Katu, hayo unayosema ndio ukweli wenyewe. Naomba niongezee hapo ulipowaongelea hao wanaoitwa viongozi.

Mara kwa mara hao ndio wanasafiri nje ya nchi. Wanapita katika viwanja vya ndege kama Schiphol (Amsterdam), Narita (Japan), JFK (New York), Heathrow (London), O'Hare (Chicago), Frankfurt, na kadhalika. Humo kuna maduka makubwa yanayouza vitu mbali mbali, vikiwemo vitabu.

Hao vigogo wetu ni wazi kuwa hawapiti kwenye maduka ya vitabu. Ingekuwa wanapita na kununua, wangeweza kupeleka angalau kamusi ya ki-Ingereza kwenye sekondari ya kata kule wilayani kwao.

Akili hiyo haimo katika vichwa vya hao vigogo. Wananunua mikufu ya dhahabu, pafyumu, na vipodozi, kwani mkorogo ni kipaumbele cha jamii yetu.

Wananunua mizinga ya "whisky." Nimeshapanda ndege na vigogo hao kuelekea Tanzania, wao wakiwa wamebeba mizinga ya "whisky."

Kwa hivi hali ndio hiyo. Kazi kubwa ya ujenzi wa Taifa ni kunywa.

Fadhy Mtanga said...

Prof Mbele kwani hujawahi kusikia hapa Tanzania hata harusi ikiwa haina pombe huwa na mahudhurio madogo sana? watu husema, "harusi gani ya kilokole hiyo nikapoteze muda?"

hata rafiki yako wa siku nyingi siku mkikutana online kisha mkapanga miadi ya kukutana, mahali ni baa.

baada ya kazi badala ya kurudi nyumbani, mahali ni baa.

pombe, pombe, pombe.

hivi ndivyo tulivyo. kama ndivyo tulivyo, tutaupata wapi wasaa wa kuyafikiria mambo ya msingi kwa kina?

SIMON KITURURU said...

Katika tembea zangu sijaona walevi kama Wafini na Warusi !
Na naongea kama mnywaji mie mwenyewe!:-(

Ila nachosifu hasa Wafini!

Wakisha kunywa kisawasawa kesho yake wako bize kazini kuliko hata WABONGo niwajuao ambao hawagusi kinywaji . Na kesho hiyohiyo unaweza kukuta wakati wanaenda kazini na wanarudi nyumbani safari nzima wameshikilia kitabu wanajisomea na fulu no kuongea na mtu!:-(


Kwa hiyo labda Pombe sio Tatizo kihivyo kwa waijuiliayo!:-(

Ni mtazamo tu!

Emmanuel said...

Aksante Prof. Ninaangalia hapa Maryland, USA Pombe inavyofichwa. Yaani pa kunywea ni ndani sana na hata pa kuuzia imejificha. Ukibeba pombe hadhari umevunja sheria. Lakini kwetu kama nilisema pale wanabidii pombe imekuwa kila mahali kwahiyo ni ruksa kwa kila mtu kila mahali. Hii ni hatari sana maana wataalam wa vinywaji wanakwambia ukiwa unaiona pombe lazima ukushawishi, na zaidi sana kuwaonesha watoto na bila kuwadhibiti basi unawaharibu mapema kabisas

Mbele said...

Ndugu Emmanuel, ni kweli. Kwa hapa Marekani, kuna sheria kadha wa kadha. Kwa mfano, ndani ya gari, wakati mnasafiri, ni marufuku watu kuwa na vyupa au vikopo vyenye bia vilivyofunguliwa.

Kila jimbo lina sheria yake kuhusu umri gani vijana wanaruhusiwa kununua bia au kunywa bia. Baa zinaangalia vitambulisho. Kama mhusika hajafikia umri unaoruhusu yeye kununua au kunywa bia, hapewi.

Halafu nimeona kwenye baa za hapa kwamba kama mteja anaonekana amelewa na anayumbayumba, hauziwi bia zaidi. Anaambiwa aende akapumzike. Sijawahi kuona walevi wa hapa wakibishana na mhudumu. Nadhani pamoja na kulewa, wanajua kuwa polisi haiko mbali.

Kwetu Bongo, hata mtu akalewa hadi kugaagaa chini, akiweza tu kusema apewe bia nyingine, analetewa.

Anonymous said...

prof Mbele hiyo picha ya mtoto anayekunywa pombo nafikiri iliipata kwenye matandao wa globle publisher ilikuwa ni kwenye pati ya baharini sijui wenyewe wanaita fiest lakini kuhusu unywaji mimi ninawashukuru wazazi walionifundisha nikiwa mdogo hivyo sio limbukeni wa ulevi maana sisikwetu si unjua Rubisi lazima babu akupe kibuyu uvute na mrija safi

Janny Merit said...

Habari am Bi, kiutamaduni na Tumaini, Taasisi mkopo halali na za kuaminika na mikopo
katika sheria na masharti wazi na ya kueleweka kwa 2% kiwango cha riba. kutoka
USD $ 12,000 kwa $ 8,000,000, Euro na paundi tu. Mimi kutoa mikopo ya biashara,
Mikopo binafsi, mikopo ya wanafunzi, gari mikopo na mikopo kwa kulipa bili. kama wewe
haja mkopo una kufanya ni kwa ajili ya wewe kuwasiliana nami moja kwa moja
Katika: (merithope6@gmail.com)
God Bless You.
dhati,
Bibi: sifa Hope
Barua pepe: (merithope6@gmail.com)

Kumbuka: majibu yote upelekwe kwa: (merithope6@gmail.com)

Bob Britten said...

Siku njema,
Je, unahitaji haraka mkopo kuanza
up biashara, au unahitaji mkopo
kwa refinance, Je, unahitaji mkopo kwa
kulipa deni? Je, unahitaji mkopo
kununua gari au nyumba? Kama ndiyo wasiwasi
tena, Tunaweza kukusaidia !!! mawasiliano
nasi sasa kupitia E-mail kwa haraka yako
mkopo.
E-mail:
davidadelekeloancompany@yahoo.com
Asante.
Mr David Adeleke
-