Tuesday, September 4, 2012

Itafakari Katuni Hii

Katuni hii nimeiona katika mtandao wa Facebook. Inamwonyesha mchora picha na mteja wake. Huyu mteja ni mu-Islam anayeonekana amekaa kwenye kochi, akiwa ameshika ua.

Mwangalie mteja huyu na halafu angalia picha iliyochorwa.

Nimeitafakari picha hii na bado naitafakari. Ninaona ina mengi ya kutufundisha. Je, mdau una maoni gani?

2 comments:

Mbele said...

Wadau, nitasema, kwa ufupi, kwa nini niliiweka katuni hii hapa. Niliiona kwenye ukurasa wa Facebook, ambako wa-Islam waliilalamikia kuwa ni mfano wa namna wa-Islam wanavyochorwa vibaya na kiuhasama na vyombo vya habari.

Nami nasema ni kweli kuwa kuna vyombo vya habari vingi mahali kama Marekani na Ulaya, ambavyo vinafanya huu uhasama dhidi ya wa-Islam.

Papo hapo, nataka kuongezea jambo moja, kwamba dosari hii ya kuwachora vibaya wengine haijitokezi kwa namna hiyo ya kuwahujumu wa-Islam tu.

Angalia Tanzania. Mimi m-Kristu nashuhudia kila kukicha jinsi baadhi ya wa-Islam wanavyotuchora kiuhasama. Wa-Islam hao wamejiaminisha kwamba wa-Kristu ni watu wabaya. Wametunga dhana ya "mfumo Kristo" ili kueneza propaganda yao hii.

Wa-Islam hao wanaeneza chuki za wazi hasa kuhusu sisi wa-Katoliki. Huwa najiuliza, je ni kweli kuwa sisi wa-Katoliki tuna roho mbaya dhidi ya wa-Islam, kama inavyodaiwa?

Kifupi ni kwamba, wale wa-Islam waliolalamikia katuni hii kwa kuwachora kiuhasama wana haki ya kufanya hivyo, nami nawaunga mkono. Papo hapo, ombi langu kwao ni kuwa waangalie pia hujuma zinazofanywa na baadhi ya wa-Islam wa Tanzania, wanapotuchora wa-Kristu, hasa wa-Katoliki, kuwa ni watu wenye chuki na wa-Islam.

Je, mdau unasemaje?

tz biashara said...

Profesa Mbele habari za siku nyingi maana nilikuwa safarini na sijaingia kwenye internet muda mrefu.

Kwakweli hii picha ni picha ambayo nimeipenda sana kwasababu inatupa au kutujengea maoni ya kuhusu ule usemi unaosema "double standard"

Nikianza na picha yenyewe inamzungumzia kijana wa kislamu akiwa anachorwa lakini hapewi picha yake ya ukweli na kinachoendelea kutoa picha ya uongo.Hivo kuihamasisha dunia kwa kutumia picha ya uongo ambayo inatumika duniani kote na ndio maana nikatumia double standard lakini mimi sio mjuzi wa lugha nauhakika utanisahihisha kama nimekosea.

Nikija katika usemi wako profesa kuhusu hujuma zinazotolewa na waisilamu dhidi ya mfumo kristo.Na hii vilevile inaweza ikawa katika usemi uleule wa double standard kutokana na hujuma zenyewe.

Lakini hakuna sehemu utakawenda na kukuta jamii ni wazuri100% ni lazima utakuta baadhi ni wahalifu,wauaji,mafisadi,wasaliti,waongo na hata wabaguzi.Ukichunguza utakuta kote kote ktk uisilamu na ukristu wapo.

Kwahio Profesa wapo waisilamu wenye ubaguzi na wapo wakristo wenye ubaguzi isipokuwa kama tumebahatika kuwa na uwelewa wa kimaisha basi tunaweza kuisaidia jamii jinsi ya kujirekebisha na kuondoa dhana potofu.

Mshindi wa maisha ni yule anaekuwa mkweli na sio msaliti wala kujivutia upande wake pale anapoona makosa kwa jamii yake.Mshindi wa maisha vilevile ni yule anaemnyenyekea mwenyezimungu kwa haki na mwenye kutenda haki na kuepusha shari.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...