
Kitabu ni rafiki ambaye yuko kwa ajili yako muda wowote unapomhitaji. Kitabu kinaweza kuwa mshauri wako, kiongozi wako, nguzo ya kuitegemea.
Akili ya binadamu inahitaji matunzo, sawa na bustani. Bustani inahitaji kurutubishwa na kupaliliwa. Ikiachwa ivamiwe na magugu, inageuka kichaka. Kusoma vitabu ni kurutubisha akili na kuipalilia. Kama mtu anaweza, ni muhimu kusoma vitabu vya aina mbali mbali: vya siasa, saikolojia, fasihi, sayansi, maisha ya watu maarufu, falsafa, historia, uchumi, na kadhalika.
Ni makosa kudhani kuwa kusoma vitabu kunawahusu wanafunzi na waalimu pekee. Kila mtu anapaswa kusoma vitabu. Tutafakari manufaa yake kwa afya ya akili ya binadamu kama yalivyoelezwa kwa ufupi katika makala hii.
No comments:
Post a Comment