Tuesday, June 18, 2013

CHADEMA: Mlipuaji wa Bomu la Arusha ni Polisi

Baadhi ya kauli za Mheshimiwa Mnyika katika video hii zinaendana na kauli aliyotoa mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, miezi kadhaa iliyopita, kwamba kuna viongozi katika CCM ambao hutumia polisi kuwahujumu wapinzani. Kwa vile mwenyekiti wa CCM alisema hivyo, nawajibika kusema kuwa ni ukweli. Bila upendeleo, nilivyomwelewa mimi ni kuwa alikuwa na nia ya kuwakanya CCM waache ufedhuli huo.

Nasubiri kusikia kauli ya msemaji yeyote wa CCM kuhusu hilo suala. Wakisema kuwa CHADEMA inadanganya, basi waseme pia wazi wazi kuwa mwenyekiti wa CCM naye ni mdanganyifu.

No comments: