Thursday, June 20, 2013

Pinda Awaagiza Polisi Kuwapiga Wakaidi

Sijawahi kusikia kutoka kwa serikali nchini Tanzania kauli kama hii ya waziri mkuu Pinda, kuwa wanaofanya ukaidi wapigwe, kwani eti nchi inaendeshwa kwa misingi ya sheria. Pinda anawaagiza polisi wawapige watu wa aina hiyo. Hapo naona Pinda anajikanyaga, kwani kama Tanzania inaendeshwa kwa misingi ya sheria, sidhani kama sheria inaruhusu kuwapiga hao anaowaita wakaidi. Vile vile maagizo ya Pinda ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kazi ya polisi ni kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha kwenye sheria. Hao ambao Pinda anawaita wakaidi wana haki ya kuhesabiwa hawana hatia hadi mahakama iamue vingine. Kuna tangazo la kimataifa la haki za binadamu ambalo liko wazi kuhusu suala hilo. Kwa muda wote tangu wanapofanya huo ukaidi hadi wanapofikishwa mahakamani, na hadi mahakama itoe uamuzi, hao watu ni watuhumiwa tu.  Huu ndio utawala wa sheria na ni msingi mojawapo wa haki za binadamu. Kusema wapigwe ni kutetea ukiukwaji wa haki za binadamu.

2 comments:

Anonymous said...

Huu ndio mtazamo wa viongozi wetu, hawana upeo kabisa.Pinda amejisahau kupitiliza hivi anadhani atakuwa waziri mkuu maishayake yote. Pinda anadhani yeye si mwanadamu na ameshushwa angani.
Huu ubabe ndio unaooleta machafuko siku kila siku, ni seme wazi tu kuwa siku watu wakianza kulipiza kisasi, itakuwa ni balaa.
Kwa maana kutokana na chuki iliyojengeka wananchi wakawaida wanawachukia sana viongozi.

Anonymous said...

Huyu jamaa ni janga na ni kama mhe shimiwa mbilinyi alivyosema hakukosea kabisa. Haelewi anachokisimamia,dunia inabadilika kwa kasi ya ajabu. Muda ni mwalimu mzuri sana, ngoja tuone mwisho wake.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...