Kwanza sio ndege wa aina zote wanaruka zao ukijaribu kuwasogea. Kuna aina ya ndege ambao wana subira. Hao ni rahisi kuwapiga picha.
Katika ujumbe wangu wa juzi, sikufafanua suala hilo. Kwa hivi, leo narekebisha kauli yangu.
Jambo jingine ambalo nimejifunza ni kuhusu matumizi ya "zoom" kwenye kamera. "Zoom" ikielekezwa kwa ndege peke yake, halafu akakuzwa sana bila kitu kingine pembeni, inapotosha ukubwa au udogo halisi wa ndege huyu. Ndege mdogo kabisa anaweza kuonekana mkubwa kama kuku.
Kwa hiyo leo nimejaribu kuwaonesha ndege wakiwa katika mazingira yao ili ukubwa au udogo wao ufananishwe na nyasi zinazowazunguka, au majani, au vijiti.
No comments:
Post a Comment