
Huyu bwana aliyeshika kitabu changu ni mwanasheria. Aliweza kuongea na baadhi ya wanafunzi, wakamweleza manufaa ya kitabu hiki kwao. Ninayo video inayowaonyesha wakiongea. Hao akina mama wawili, mmoja mwenye khanga na mwingine mwenye "jeans" ni mahakimu.
7 comments:
Profesa,
hongera kwa kufundisha kwa vitendo
Kitabu hiki nilimwazima msomaji mmoja mwenye njaa ya maarifa...hakufanikiwa kukirudisha zaidi ya mwaka sasa. Nitatafuta nakala nyingine niweze kukirudia. Najisikia fahari kuwa kimeandikwa na Mtanzania.
Asante, Ndugu Bwaya, kwa yote uliyonena. Pole kwa kupotelewa kitabu chako. Hata hapa Marekani, watu wameniandikia kuwa wameazimisha nakala zao na katika kuzunguka kutoka kwa huyu hadi yule, kitabu hakijulikani kiliko. Imewabidi kuagiza nakala nyingine.
Ukiniletea anwani yako ya posta, nitakuletea nakala nyingine, ya bure, kwa heshima yako.
Profesa,
Nimepata faraja kujua kuwa tukio la kupotelewa kitabu hiki ni tatizo la wengi. Kwa hakika nina uhakika hata aliyekiazima kwa aliyekiazimisha kwangu, naye kaazimisha kwa mwingine asiyejua aliyenacho kwa sasa. Ni mali. Ni maarifa.
Sasa naomba kuchangamkia ofa hii. Anuani yangu ni:
Christian Bwaya,
School of Education,
University of Dar es Salaam,
P.O. Box 35048
DAR ES SALAAM
Nakingoja kwa shauku kubwa :)
Ndio ninatoka posta kusafirisisha kitabu.
Profesa,
Sina maneno sahihi ya kushukuru kwa ofa hii maalum. Asante sana sana kwa kujali kiu yangu ya kuelimika. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa kutumia muda wako kusambaza elimu.
Nikikipata tu, nitakujulisha.
Wewe na mimi tunafanana kwa hiyo unayoiita kiu ya kuelimika. Sina la kuongeza hapo, bali niseme tu kuwa mwenye masikio asikie.
Tuombe kila kitu kiende tunavyotegemea, yaani kitabu kikufikie. Kila la heri.
Post a Comment