Wednesday, July 16, 2014

Madreva Wetu Katika Kozi ya "Hemingway in East Africa, 2013"

Katika safari zetu, wanafunzi wangu nami, nchini Tanzania, mwezi Januari mwaka 2013, tulitumia kampuni ya utalii ya Shidolya, yenye makao yake Arusha. Hapa naleta picha ya madereva wetu, kutoka kwenye kampuni hiyo.

Tulisafiri salama kila mahali: Arusha, Longido, Mto wa Mbu, Karatu, Ngorongoro, Serengeti, Manyara, Babati, na Tarangire. Tulikuwa na bahati; hatukupata tatizo.

Nimeona ni jambo jema kuwakumbuka madereva. Kwa bahati mbaya sina picha ya wapishi wetu, ambao nao walituhudumia vizuri kabisa.

No comments: