Tuesday, July 1, 2014

Ngorongoro

Hapa ilikuwa ni mwezi Januari, 2013. Niko katika bonde la Ngorongoro, mmoja ya vivutio vikubwa vya utalii Tanzania. Nimebahatika kufika sehemu hiyo mara kadhaa. Kila wakati naguswa na uzuri na upekee wa mahali hapo.Mara ya kwanza kufika hapo nilikuwa kiongozi wa wanafunzi na wazazi wao kutoka shule ya Shady Hill, Boston. Nilikuwa nimeombwa na kampuni ya Thomson Safaris kuongoza msafara huu.Miaka iliyofuata nimefika hapo na wanafunzi kutoka vyuo vya Marekani vya Colorado na St. Olaf, tukiwa katika kozi ya "Hemingway in East Africa," ambayo niliitunga. Nimeandika makala kadhaa kuhusu kozi hiyo, na makala ya hivi karibuni kabisa ni hii hapa

Kila wakati naguswa na uzuri na upekee wa mahali hapo. Kuna wanyama wa aina aina, kama vile samba, pundamilia, twiga, tembo, vifaru na nyati.

Mara zote, tulitembelea pia hifadhi za Serengeti, Manyara, na Tarangire. Zote hizo ni utajiri mkubwa wa nchi yetu, kwa sasa na kwa vizazi vijavyo.

No comments: