Tuesday, July 8, 2014

Karatu: Baada ya Darasa Kumalizika

Hapa ni Karatu, Tanzania, mwezi Januari, mwaka 2013.  Ilikuwa mara tu baada ya kumaliza kipindi katika kozi yangu ya "Hemingway in East Africa." Hapa wanaonekana wanafunzi, mimi, na wenyeji watatu waliokuja kujumuika nasi. Sote tulifurahi kujumuika nao.

Huyu bwana aliyeshika kitabu changu ni mwanasheria. Aliweza kuongea na baadhi ya wanafunzi, wakamweleza manufaa ya kitabu hiki kwao. Ninayo video inayowaonyesha wakiongea. Hao akina mama wawili, mmoja mwenye khanga na mwingine mwenye "jeans" ni mahakimu.

7 comments:

Christian Bwaya said...

Profesa,

hongera kwa kufundisha kwa vitendo

Christian Bwaya said...

Kitabu hiki nilimwazima msomaji mmoja mwenye njaa ya maarifa...hakufanikiwa kukirudisha zaidi ya mwaka sasa. Nitatafuta nakala nyingine niweze kukirudia. Najisikia fahari kuwa kimeandikwa na Mtanzania.

Mbele said...

Asante, Ndugu Bwaya, kwa yote uliyonena. Pole kwa kupotelewa kitabu chako. Hata hapa Marekani, watu wameniandikia kuwa wameazimisha nakala zao na katika kuzunguka kutoka kwa huyu hadi yule, kitabu hakijulikani kiliko. Imewabidi kuagiza nakala nyingine.

Ukiniletea anwani yako ya posta, nitakuletea nakala nyingine, ya bure, kwa heshima yako.

Christian Bwaya said...

Profesa,

Nimepata faraja kujua kuwa tukio la kupotelewa kitabu hiki ni tatizo la wengi. Kwa hakika nina uhakika hata aliyekiazima kwa aliyekiazimisha kwangu, naye kaazimisha kwa mwingine asiyejua aliyenacho kwa sasa. Ni mali. Ni maarifa.

Sasa naomba kuchangamkia ofa hii. Anuani yangu ni:

Christian Bwaya,
School of Education,
University of Dar es Salaam,
P.O. Box 35048
DAR ES SALAAM

Nakingoja kwa shauku kubwa :)

Mbele said...

Ndio ninatoka posta kusafirisisha kitabu.

Christian Bwaya said...

Profesa,

Sina maneno sahihi ya kushukuru kwa ofa hii maalum. Asante sana sana kwa kujali kiu yangu ya kuelimika. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa kutumia muda wako kusambaza elimu.

Nikikipata tu, nitakujulisha.

Mbele said...

Wewe na mimi tunafanana kwa hiyo unayoiita kiu ya kuelimika. Sina la kuongeza hapo, bali niseme tu kuwa mwenye masikio asikie.

Tuombe kila kitu kiende tunavyotegemea, yaani kitabu kikufikie. Kila la heri.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...