Ukiwa mjini Mbamba Bay, hoteli hii inaonekana vizuri, kwani iko kilimani. Ukiwa hapo hotelini, unaliona Ziwa Nyasa vizuri na mji wa Mbamba Bay chini yako.
Hoteli hii ni nzuri kwa kila hali, kuanzia mazingira hadi huduma za malazi na chakula. Ni aina ya hoteli ambayo unategemea kuiona katika miji mikubwa, si mji mdogo kama huu.
2 comments:
Nakubaliana na Prof. Ni hotel nzuri kwa kweli nimewahi kuwa hapa..
Masista waliona mbali. Sasa Mbamba Bay imekuwa makao makuu ya wilaya ya Nyasa, nadhani mradi wao huu utapanda chati.
Post a Comment