Wednesday, September 28, 2011

Safari ya Madison, Kuongelea Kitabu

Naandika makala hii nikiwa katika gereji ya Car Time, mjini Northfield, Minnesota. Nimeleta kijigari changu kichekiwe, ili kesho nikiendeshe kwenda Madison, Wisconsin, kuongelea kitabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences.

Kwa wanaopenda kufahamu zaidi masuala haya, ni kwamba huku Marekani, ukiandika kitabu kinachowagusa watu, utegemee kupata mialiko ya kwenda kuongelea kitabu hicho.

Shughuli ya kukutana na wadau namna hii inategemea aina ya kitabu. Kama ni riwaya au kitabu cha mashairi, unategemewa kusoma visehemu vya riwaya au mashairi hayo. Kama ni kitabu cha elimu jamii kama hicho changu, sio lazima kusoma sehemu yoyote. Watu hupenda kusikia maelezo ya yatokanayo na ulichoandika, na pia uyajibu au kuyajadili masuali yao.

Hapa Marekani, watu wanapenda kuwasikiliza waandishi kwa namna hizo nilizoelezea. Wanamlipia mwandishi usafiri, malazi, na ruzuku, bila kusita, ili waweze kumsikia.

2 comments:

Simon Kitururu said...

Kila la kheri na SAFARI NJEMA!
-MDAU

Mbele said...

Shukrani kwa baraka zako. Nitajitahidi niwezavyo kuongea na kufafanua masuala vizuri kabisa. Si unajua tena, unapokuwa katika hali kama hii, wasikilizaji wanakuona wewe sio kama wewe tu, bali mwakilishi wa nchi yako. Hapo ndipo ngoma ilipo :-)

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...