Monday, September 26, 2011

Ziara ya Lyulilo, Ziwa Nyasa

Ukifika Matema Beach, Ziwa Nyasa, hutakosa kusikia kuhusu vijiji vya jirani, kama vile Lyulilo na Ikombe. Nilikuwa maeneo hayo tarehe 20 Agosti mwaka huu katika msafara wa programu ya LCCT, kama nilivyoelezea hapa.

Hapa kushoto ni Matema Beach, ambapo unapata mtumbwi wa kukuvusha hadi Lyulilo. Hapa mwendesha mtumbwi anaandaa safari. Nauli ni makubaliano.










Safari inaendelea. Hatukukumbana na mawimbi wala usumbufu mwingine.












Kadiri dakika zinavyopita, Lyulilo inazidi kuonekana vizuri.













Hapa sasa tumekaribia sehemu ya kutua.












Baada ya kutia nanga, tunaingia mitaani Lyulilo. Ni siku ya soko. Watu wamejaa kila mahali katika mtaa mkuu wa Lyulilo.


























Kuna bidhaa tele, kama vile vyungu. Lyulilo ni maarufu kama soko la vyungu, ambavyo hutengenezwa na wafinyanzi katika kijiji cha Ikombe, mbele kidogo ya Lyulilo. Hatukufika
Ikombe; nategemea mwakani, Insh'Allah.






















Hapo kushoto wanaonekana wauzaji na wateja wa pombe za kienyeji. Mzee mwenye kiko alisisitiza nimpige picha vizuri ili kiko kionekane.











Hiyo ni fursa ya wenyeji kukutana na wageni.

No comments:

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...