
Nyumbani ni nyumbani. Leo nimeikumbuka Songea, nikaamua kuleta picha mbili tatu nilizopiga mwaka huu. Hapa kushoto ni barabara itokayo stendi kuu kuelekea bomani, hatua chache tu kutoka duka la vitabu la Kanisa Katoliki. Nyuma ya haya majengo ndipo kilipo
Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki.
Hapa ni taswira ya uwanja wa Maji Maji, kutoka juu. Nilipiga picha hii kutoka ghorofa ya tatu ya hoteli niliyofikia, ng'ambo ya barabara kutoka kituo kikuu cha polisi. Kule ng'ambo ni kitongoji cha Lizaboni, njiani kuelekea
Peramiho,
Mbinga, na
Mbamba Bay.

Hapa kushoto ni stendi kuu nikiwa na dada yangu na mdogo wangu.
No comments:
Post a Comment