Saturday, February 14, 2015

Miaka Kumi ya Kitabu: Shukrani Wanablogu

Katika kusherehekea miaka kumi tangu nilipochapisha kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, nawajibika kuwakumbuka watu wengi waliokuwa nami bega kwa bega katika kunitangazia kitabu hiki. Leo napenda kuwakumbuka wanablogu wa ki-Tanzania, ambao wamechangia katika kunihamasisha na kuniunga mkono miaka yote hii.

Pichani hapa kushoto anaonekana mwanablogu Simon Kitururu, ambaye amewahi kuniambia mara kadhaa kuwa anasoma maandishi yangu kila yanapopatikana. Anaonekana ameshika vitabu vyangu viwili: Matengo Folktales na Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Picha hiyo aliichapisha katika blogu yake ya Mawazoni.

Mwanablogu Issa Michuzi amefanya juhudi kubwa kutangaza shughuli zangu, kama vile warsha na mihadhara. Ni mfuatiliaji wa blogu yangu, na mara kwa mara huamua kuchapisha baadhi ya makala zangu katika blogu yake. Hata leo amechapisha makala yangu kuhusu kitabu changu kutimiza miaka kumi.

Subi Nukta naye ametoa mchango wake, ikiwemo kutangaza kitabu hiki kinachotimiza miaka kumi. Katika blogu yake, aliandika hivi:

Africans and Americans: Embracing Cultural Differences is a book by Professor Joseph Mbele that I would recommend to anybody willing to learn something about a culture that is different fro theirs.

Since Tanzania is my home country, I'd ask anybody planning to travel to Tanzania, or anybody unsure on what to do when in a different culture to buy this book. To order your copy, simply click on the book's image and you will be taken to lulu.com where you can purchase it
.

Jeff Msangi ni mwanablogu mwingine ambaye ananiunga mkono kwa dhati. Aliandika kuhusu kitabu changu hapa. Hakuishia hapo, bali siku nyingine alandika hivi:

Now, if you live or have lived in the US in the past, you will agree with me that there are a lot of things or let me call them cultural differences between Africans and Americans. There is a lot of learning and adjustment for newcomers/immigrants from Africa. The same applies to Americans going or rather growing up in Africa. My good friend, Prof. Joseph Mbele, highlights these cultural differences very well in his famous book titled “Africans and Americans-Embracing Cultural Differences”. I recommend everyone to read this book.

Christian Bwaya ameandika mara kadhaa kuhusu kitabu hiki, kwa mfano hapa. Wanablogu wengine wametoa mawazo yao kuhusu kitabu hiki katika maoni kwenye mijadala. Mfano ni Sophie Becker ambaye aliandika katika blogu ya Jielewe:

Hiki kitabu kifundisha na kuburudisha. Kinakuelezea mambo ambayo yangekuchukua miaka kadhaa kuyaelewa au usiyaelewe kabisa harafu Prof.Mbele kakiandika with sense of humor utacheka sana.nimekipenda sana.

Ningeweza kuendelea kuwataja wanablogu wengine, kama vile Rachel Siwa Isaac, Profesa Masangu Matondo, na Yasinta Ngonyani, ambaye aliandika maoni yake hapa. Naamini kuwa wanablogu niliowataja na hata ambao nimeshindwa kuwataja, hawajaishia kuandika tu kuhusu kitabu changu. Bila shaka, kama ilivyo ada kwetu wanadamu, wamekiongelea na wanakiongelea katika mazingira mengine pia, kwa marafiki na watu wengine. Ninawashukuru wote kwa kuniunga mkono katika jukumu hili la kujenga mahusiano mema baina ya watu wa tamaduni tofauti.

2 comments:

Mfuko said...

Hongera sana Prof Mbele kwa hatua hii kubwa ninafuraha kukufahamisha nimekipata kitabu hiki jana jioni sana Zaidi kila ukurasa ninao fungua ni elimu iliyojitoshelezea hasa nikiwa muhusika ktk jamii hizi mbili kwa kuishi hapa marekani na kuzaliwa na kukulia Africa.Hongera

Mbele said...

Ndugu Mfuko,

Shukrani sana kwa ujumbe wako. Ninakukumbuka vizuri, kutokana na mawasiliano yetu kuhusu kile kitabu cha "A Dream is a Goal With a Deadline."
Ingawa wakati ule sikukuelewa vizuri, ninaanza kutambua kuwa uko makini na masuala haya. Nami niliandika kitabu changu kutokana na hali halisi ya kuishi na wa-Marekani, kama unavyoona, ili kuwasaidia wengine.

Nakutakia kila la heri.