Thursday, March 5, 2015

Kofia Katika Mazishi ya Ki-Katoliki

Niliona taarifa za msiba na mazishi ya Kapteni John Komba mitandaoni. Ni jambo la kushukuru kwamba waandishi na wapiga picha walituwezesha tulio mbali kuelewa mambo yalivyokuwa.

Nilivyoona picha inayoonekana hapa kushoto, ya jeneza likiteremshwa kaburini, niliamua kuandika ujumbe katika blogu ya Michuzi nikisema kuwa nimekerwa na kitendo cha wahusika kuwa wamevaa kofia wakati wa shughuli hiyo. Niliuliza iwapo jambo hili linaruhusiwa kwa mujibu wa ibada za mazishi ya ki-Katoliki.

Akina "anonymous" kadhaa wamejitokeza na kuandika hili au lile, katika sehemu ya maoni. Nami katika sehemu ile ya maoni, nimejaribu kuelezea zaidi suala langu, nikisema, kwa mfano, kuwa kwa askofu kuvaa kofia ya kiaskofu wakati wa kuendesha ibada ni sehemu ya mavazi yake rasmi ya ibada.

Sikuona kama duku duku yangu imejibiwa. Badala yake, niliona watu wanazua mambo ambayo hayahusiani na ulizo langu, ulizo ambalo lilitokana na nia njema, yaani kujiridhisha kuwa tunaheshimu ibada na tunamheshimu marehemu.

Nimeamua kuhamishia suali langu hapa kwenye blogu yangu. Ningependa kusikia maoni ya wa-Katoliki wenzangu, ambao wana ufahamu zaidi yangu kuhusu uvaaji wa kofia wakati wa ibada ya mazishi ya ki-Katoliki.

8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nipo nawe Prof. Kofia hairuhusiwi kabisa kwa ninavyofahamu mimi kama mkatoliki. Huruhiwi kuvaa kofia kanisani na wala kwenye ibada yoyote ile. Halafu kumbukeni pia hata wakati wa kula chakula huruhusiwi kuvaa kofia

Anonymous said...

Nakumbuka nikiwa mtumishi(ministrant) miaka kumi na tatu iliyopita, askofu alikuwa anavaa kofia ndogo wakati wa mageuzo, na wakati wa mwigine uliobakia ile kubwa.
Kwa mtazamo wangu ni kuwa;
Kofia ni sehemu ya mavazi, na inaonesha mamlaka aliyopewa. Sidhani kuvaa au kutokuvaa kofia kama ni kosa. Ila sasa inategemea umetoka katika utamaduni upi. Mfano kwa wamarekani kuvua kofia hutumika kuonesha heshima au kukubali kitu au hoja wakati wa mazungumzo.
Kwa Wachina, mwanaume hanunuliwi au kupewa kofia kama zawadi.
Mwisho nahitimisha kwa kusema, sidhani kama kuvaa au kuvaa kofia kwa watanzania ni kitu cha maana sana katika utamaduni wetu. Kwani kofia haijawahi kuwa sehemu ya utamaduni wetu au sehemu ya mavazi yetu. Hivyo tunapozungumza haya inategemea upo wapi. Kumbuka kurejea hoja ya utamadunisho.

Anonymous said...

Kwa kuongezea katika utamadunisho. Nimezunguka katika nchi mbali mbali duniani za asia na ulaya, kwa kunatofauti ndogo ndogo kwa jinsi waumini na kanisa linapofanya ibada au misa. Mfano kitu ambacho nilikona katika baadhi ya makanisha india waumini huvua viatu waingiapo kanisani. Ukienda afrika nyimbo za ibada huchanganya na ngoma na na si ajabu mapadri kuvaa mavazi ya vitenge.
Ulaya niliona wakitumia magitaa kanisani na ilikuwa kawaida waumini kutoa mahubiri baada ya neno. Nionavyo hoja ya kofia si kitu sana, inategemea na utamaduni uliopo na ILA tu kama haibadili mafundisho ya msingi, maadili na ustaarabu wa kanisa.
Kwa uzoefu niliouona, mazingira na uelewa wa waumini hutofautiana mahali na mahali. Hivyo swala la kuvaa kofia au kutokuvaa kofia si la muhimi sana kwa baadhi ya watu.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Kuondoa ubishi nadhani kila mtu angejenga na kutetea hoja yake kwa ushahidi wa maandiko au kanuni za dhehebu husika. Binafsi sina la kuchangia zaidi ya kuendelea kusoma maoni ili nijifunze hili na lile. Ila kwa kumbukumbu yangu wanaovaa kofia ni mayahudi na Waislamu ukiachia mbali masingasinga, Akolino na baadhi ya madhahabi kuvaa vilemba. Kwa wakristo wawe wasabato, Waroma Walutheri na wengine wengi sikumbuki kuwaona wamevaa kofia wakielekea kwenye majengo yao ya ibada. Bahati mbaya mi na kitu hii mbali mbali hasa pale Mungu alipojificha. Anyways tuyaache haya.

Mbele said...

Nashukuru kwa moyo wenu wa kuchangia suala hili, ambalo limenikera.

Lengo langu ni kufahamu kama kofia zinaruhusiwa katika ibada ya mazishi ya ki-Katoliki.

Labda nifafanue kwa kusema kuwa naongelea ibada ya mazishi ya ki-Katoliki kama inavyofanyika Tanzania. Je kofia zinaruhusiwa?

Siongelei madhehebu mengine, dini zingine, nchi zingine, tamaduni zingine, au mavazi kwa ujumla. Naongelea uvaaji wa kofia kwenye ibada ya mazishi ya ki-Katoliki nchini Tanzania.

Nimesema kuwa askofu wa kanisa Katoliki anapoendesha ibada, anatakiwa kuvaa kofia yake rasmi. Lakini je, watu wengine, kama hao wanaoonekana pichani, wanaruhusiwa?

Anonymous said...

Saihihisho: Hapo kwa wachina ni kofia ya kijani

Unknown said...

Vipi kwa Mimi muislamu ninapoenda kushiliki mazishi ya mkristo mroma nami kuvaa kofia yani baraghashia ni Sina kwangu .je ninapoenda kuzika natakiwa kuvua kofia?

Mbele said...

Ndugu Muislam, suali lako naliona murua sana. Mimi naona itakuwa muafaka sana Muislam kuvaa kofia yako kwenye mazishi yetu waKatoliki, kwani utakuwa umejikita katika ibada ya dini pia. Huu ni mtazamo waangu.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...