Tuesday, March 10, 2015

Mdau Anauliza Kama Ufisadi Utaisha Nchini

Mdau anonymous ameomba tusome makala ifuatayo na ameuliza iwapo ufisadi utaisha Tanzania.

Makala aliyoleta inamhusu Dr. Fulgence Mosha, anayeonekana pichani, daktari bingwa mstaafu wa hospitali ya KCMC, ambaye amekuwa akihangaikia mafao yake ya ustaafu kwa miaka kumi bila mafanikio. Makala aliyoileta mdau ni hii hapa.

7 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Inasikitisha na kuchukiza ukiachia mbali kuwa kichocheo cha ufisadi kwa wale walioko makazi kwa kuchelea kuwapata kilichomfika daktari huyu maskini. Nadhani mchango wake kwa taifa ni mkubwa kuliko hata hao akina Kikwete na genge lake la wezi na mafisadi wanaotumbua kwa mikono na miguu tena bila kuomba wala kunawa. Je tunalipeleka wapi taifa namna hii? Hata hivyo, kuna siku wanaowatenza watu wema hivi wataaibika tu. Maana malipo ni hapa hapa duniani. Tumeona akina Gbagbo, Saddam, Gaddafi na wengine wengi waliojifanya miungu walivyoumbuka. Hii ni dhuluma amabayo haina mfano.

Anonymous said...

Utawala mbovu ni zaidi ya ukoloni, kwa mfanyakazi yoyote akiona hii habari hawezi kuwa na imani na mfumo mzima wa hifadhi ya jamii. Na mwishowe kuanza kujitajirisha kabla hayajamkuta.

Mbele said...

Napenda kuongelea juu yangu mwenyewe. Tangu nilipoanza kuajiriwa, kufundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 1976, nilifanya kazi kwa bidii na uadilifu mkubwa. Nilimtendea haki kila mwanafunzi, bila upendeleo wala dhuluma, wala rushwa, si mwanamke si mwanamme, si Muislam, m-Kristu, au asie na dini.

Ninathibitisha kuwa huu ndio ukweli, na hakuna mwanafunzi au yeyote mwingine anayeweza kudai na kuthibitisha vingine.

Lakini, baada ya miaka kupita, nilikutana na matatizo yaliyosababishwa na taratibu za kiutawala, hadi nikaondoka kabisa pale. Sitaki kuongelea hapa undani wa jambo hilo, ila baada ya kuondoka, siku moja nilitanguzana na rafiki yangu, mhadhiri mwenzangu, Dr. Kulikoyela Kahigi (ambaye sasa ni Mbunge wa Bukombe, CHADEMA)tukaenda kwa Profesa Issa Shivji kumwuliza kuhusu suala langu. Alituambia kuwa Chuo kilikuwa kimenikosea haki na kuwa ningeweza kwenda mahakamani ila tu nilichelewa mno, kwa mujibu wa sheria nimekuwa "time-barred."

Chuo kama kingekuwa kinajali utumishi wa mwajiriwa, hakingeniweka katka mtego, bali kingeniongoza njia ya haki. Matokeo yake ni kuwa sikupata hata senti moja ya mafao ya utumishi wangu.

Mfuko said...

Pole sana Mzee Mbele, unakatisha sana tamaa huu mfumo mzima wa hifadhi ya jamii wa Tnzania.

Mbele said...

Ndugu Mfuko

Shukrani kwa ujumbe. Binafsi, ninapenda kumsikia yeyote anayelalamika aanze kwanza kuthibitisha kuwa yeye ni tofauti na wale anaowalalamikia. Athibitishe kwamba yeye ni mwadilifu, halafu ndio aanze kulalamika au kushutumu.

Tatizo moja ninaloliona ni kuwa utawasikia wa-Tanzania wanalalanika kuhusu ufisadi, na hapo wanaishia kuwataja vigogo mafisadi, kama kwamba wakiondolewa hao vigogo na kuadhibiwa, ufisadi utakuwa umefutwa Tanzania.

Kwa kifupi, nataka kusikia habari kama ya huyu Dr. Mosha, ambaye amelitumikia Taifa kwa uadilifu maisha yake yote. Huyu ana haki ya kulalamikia ufisadi. Ana haki ya kuwashutumu mafisadi.

Jambo jingine linalonikera ni kuwa jamii yetu inamwona yeyote aliyeko nje ya nchi kuwa ni mtu asiye mzalendo, mtu aliyeikimbia nchi na kwenda kujitafutia maslahi binafsi.

Kubaki nchini inakuwa ndio kigezo cha uzalendo. Hata mafisadi, ambao wako nchini, wanafaidika na dhana hiyo, na inakuwa rahisi wao kupanda majukwaani na kutukejeli sisi tulioko nje, bila kuangalia sababu zilizomfanya kila mmoja wetu kuondoka nchini.

Anonymous said...

Pole sana prof Mbele, haya yaliyokukuta yamewakuta wengi sana, tena wajene ndio usiseme. Wengi wanateseka sana na mafao ya wenzi wao ambao walifariki kabla hawajastaafu.

Watanzania tumejenga utamaduni mbaya sana, ambao moja kwa moja ndio unachochea haya yote. Utamaduni wa kutokuwajibika, kutokufuata uraratibu na kutenda chini ya kiwango.
Uwajibikaji kwa watendaji ni mdogo sana, hawa wafanyakazi wa uma, na ndio yanayochochea haya yote. Hakuna kitu kinafanyika kwa wakati.
La kutokufuata utaratibu sisi ndio tumekuwa mabingwa, hakuna kitu kinaenda ndani ya utaratibu ni lazima uchepuke.
Hili linagharama zake, mfano.
Ukienda hospitali kama humjui mtu basi kupata huduma kwa wakati lazima utoe rushwa, ukienda polisi , mahakama, vyuoni nakadhalika.
Hata hizi shule za binafsi zinazofanya vizuri, nyingi kama humjui mtu ni shida kupata nafasi ya
mwanao kusoma.
Sasa embuo ona hili la waziri hapa, anasema ili tatizo la huyu bwana litatuliwe basi amuone. Sawa, lakini kwani hakuna utaratibu?, kwanini mtu anatesema muda mrefu hivyo bila kupata haki yake?, inamaana toka awali angemjua waziri basi angepata haki yake sio.
Hili mimi binafsi linanipa shida sana, inamaana nchi ya watu millioni 46, kupata huduma basi ni sharti uwajue wafanyakazi waserekali walau 400,000.
Hii inamaana pia prof Mbele ungekuwa unamjua mtu, ungepata haki yako.

Mbele said...

Mdau Anonymous wa March 12, at 1:03 AM, shukrani kwa mchango wako, ambao unaendelea kuthibisha jinsi ufisadi ulivyozagaa katika jamii yetu.

Ni wazi kuwa mapambano dhidi ya ufisadi sherti yaanzie kwa kila mtu kujisafisha kwanza yeye mwenyewe. Bila kuwa safi, watu wanapata wapi ushujaa na uhalali wa kuwalalamikia hao wanaoitwa mafisadi?

Bila kujisafisha, malalamiko dhidi ya ufisadi ni unafiki na uwongo, kwani hauwi umejengeka katika kuuchukia ufisadi wala kutaka utokomezwe.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...