Wednesday, March 18, 2015

Neema Komba Ashinda Tuzo ya Uandishi

Neema Komba ni mwandishi chipukizi wa ki-Tanzania. Kama wewe ni mfuatiliaji wa uandishi wa Tanzania wa siku hizi, huenda tayari unafahamu habari zake. Mbali na uandishi, Neema ni mhamasishaji wa uandishi na sanaa husika kupitia jukwaa liitwalo la Poetista.

Mwaka 2011 Neema alichapisha kitabu cha mashairi yake, See Through the Complicated. Nilikisoma muda si mrefu baada ya kuchapishwa. Mwishoni mwa mwezi Julai, 2012, nilipokuwa Tanzania, tulikutana Lion Hotel, Dar es Salaam, tukaongelea uandishi wake.

Pamoja na mashairi, Neema ni mwandishi wa insha. Hivi karibuni nilianza kufahamu kuwa anaandika pia hadithi, niliposoma kuwa hadithi yake "Setting Babu on Fire" imeteuliwa kuwemo kati ya hadithi tatu zilizoteuliwa kushindania tuzo ya "Flash Fiction" ya Etisalat. Hayo yalikuwa mashindano makubwa ya uandishi barani Afrika. Hatimaye, "Setting Babu on Fire" imeshinda tuzo ya kwanza.




Ushindi huu ni sifa kubwa kwa Neema mwenyewe na kwa Tanzania. Nikizingatia kuwa huyu ni mwandishi chipukizi, lakini mwenye ubunifu wa hali ya juu na mwenye kukimudu vizuri ki-Ingereza, sina shaka kuwa nyota yake itazidi kutukuka na kung'ara miaka ya usoni. Nampa hongera sana na kumtakia kila la heri.

9 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Natamani nipate kitabu chake. Hata hivyo nampongeza maana ukiamua kuandika ujue una roho ngumu hasa kwa nchi ambako vitabu ni sehemu ya mwiko kwa wasomaji. Kaza buti mdogo wangu tunakukaribisha kwenye klabu hii ya wabukuzi na waelimishi. Shukrani kaka Mbele kumleta dada yetu katika anga ya uandishi na changamoto zake.

Mbele said...

Ndugu Mhango, mwalimu mwenzangu, tuko pamoja katika kuhamasisha usomaji na elimu kwa ujumla. Neema ni binti mdogo kwa umri, na inavutia kuona anavyojituma katika masuala ya uandishi na uhamasishaji wa uandishi na sanaa kwa ujumla.

Ni wajibu wetu sisi, ambao kwa mila zetu tunafahamika kama wazee, kuonyesha mfano na kuwahamasisha hao vijana.

Kwa bahati nzuri, kuna vijana kadhaa Tanzania, waandishi chipukizi, ambao wamenitafuta ili kupata ushauri, name naendelea na mawasiliano nao. Hatuwezi kujua, hao huenda ndio watakuwa akina Chinua Achebe wetu, akina Toni Morrison wetu, akina Shaaban Robert wetu, ambao Taifa la kesho litajivunia.

Unknown said...

Hongera sana Neema komba! Prof. Naomba address za Neema komba!

Mbele said...

Ndugu Mlengela, nitampelekea Neema ujumbe wako. Anaishi Tanzania, na mimi niko huku Marekani.

Je, ni wewe Daudi Mlengela ambaye tulikutana mwaka 2010 pale Diamond Jubilee Dar es Salaam kwenye maonesho ya Tripod Media?

Mbele said...

Ndugu Mlengela

Neema ameniletea anwani yake na amesema nikupe. Basi, nipe anwani yako. Yangu ni africonexion@gmail.com

Unknown said...

Haswaa! Ndo mie! Nitashukuru sana iwapo nitapata address zake. Address zangu ni mlengelad@gmail.com na +255714591703. Natumain zitamfikia.

Mbele said...

Ndugu Mlengela, nimeshakuletea anwani ya Neema kwa barua pepe.

Unknown said...

Habari prof. zile address za dada komba bado sijazipata, sijui Kwa nini. Nakutakia sikukuu njema ya pasaka wewe pamoja na familia yako, rafiki zako na majiran zako Siku hiyo!

Unknown said...

Nimepata! Aksante sana!

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...