Wednesday, March 11, 2015

Video ya Kumbukumbu ya Miaka Kumi ya Kitabu

Jana, binti yangu Zawadi na mimi tulirecodi video ya kumbukumbu ya miaka kumi tangu nilipochapisha kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences.

Hatukuwazia tungefanya shughuli hiyo jana. Tulijishitukiza bila maandalizi. Tulitayarisha kompyuta nami nikaanza kuongea. Zawadi alifanya shughuli yote ya kiufundi hadi kuiweka video katika
mtandao wa You Tube.

Katika kumbukumbu hii ya miaka kumi ya kitabu changu, napenda kuwashukuru wasomaji wangu, familia, na marafiki na wengine wote walionihamasisha kwa namna moja au nyingine.

Kwa mwezi huu wote, yeyote anayetaka kitabu hiki, popote duniani, ataweza kukipata kutoka kwangu kwa bei nafuu ya dola 12. Awasiliane nami kwa barua pepe, africonexion@gmail.com au simu (507) 403 9756. Mwisho wa fursa hii ni tarehe 31.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nimependa sana mtindo wako wa kukitangaza kitabu hiki. HONGERA SANA KWA KUMBUKUMBU YA MIAKA KUMI YA KITABU. TUPO PAMOJA.

Mbele said...

Shukrani, Dada Yasinta, kwa ujumbe wako. Pamoja na uandishi, huwa najielimisha kuhusu uandishi wa vitabu, kuhusu uchapishaji na uuzaji wa vitabu. Ninanunua na kusoma vitabu vinavyoelimisha kuhusu masuala hayo.

Papo hapo, ninajitahidi kuwanufaisha wengine kwa yale ninayojifunza. Kwa mfano, mara kwa mara huwa naandika makala katika blogu hii, na nimeweka pia makala katika kitabu changu cha CHANGAMOTO: Insha za Jamii, ambamo nawaeleza wengine yale ninayoyafahamu.

Hizi juhudi zangu za kutangaza kitabu change ni mwendelezo wa hayo niliyosema hapa juu. Vitabu nilivyosoma vinasisitiza mengi, na mojawapo ni jukumu la mwandishi kutangaza kitabu chake. Nami nategemea kuwa kwa kuonyesha mfano, waandishi wasiojua suala hilo wataweza kujifunza.

Mimi kama mwalimu, nina wajibu wa kufanya utafiti, kujielimisha, na kuwafundisha wengini. Kuandika Makala na vitabu ni wajibu wangu, na kama ilivyo kwa mwalimu ye yote, kazi yangu ni kuwapa wengine yale ninayoyafahamu. Kwa msingi huu, nina wajibu wa kutangaza vitabu vyangu.

Ninashukuru kuwa wasomaji nao, wanablogu kama wewe Dada, wahakiki, na walimu wenzangu hapa Marekani wamekuwa mstari wa mbele katika kunitangazia kitabu hiki na vitabu vyangu vingine.

Napenda kurudia shukrani zangu kwako.