Monday, September 12, 2011

CCM Yamwaga Wali Kwa Wapiga Kura Igunga

Chanzo: Kulikoni


7 comments:

Albert Kissima said...

kwa umasikini wa akili (na kipato pia) tulionao sisi watanzani, inawezekana kabisa tukafakamia wali na kisha tukaridhika kabisa na kugawa kura zetu kwa watu mtu asiyestahili. Watanzania walio na "myopia" ya akili, watakula wali, watashiba na wataridhika na watasubiria wagombea wengine nao kama wataleta wali. Kama hawataleta wali, bali kujadili changamoto zinazowakabili wapiga kura na suluhisho; kura hawatapata maana badala ya kuleta wali, wanaleta porojo. Wenye fikra hizi, wana myopia ya akili, na pengine bado ni wengi.

Mbele said...

Hiyo ndio Bongo. Sitashangaa iwapo atatokea mgombea atakayemwaga wali na kisha amwage bia za kuteremshia.

Anonymous said...

Mzee Mbele (Nimekuita Mzee kwa heshima kutokana na umri wako) katika picha na habari zote ulizoziona kwenye mablogu wiki hii hiyo picha ya chakula ndio umeiona ya maana? Ina maana hufahamu kuwa tuko katika maombolezo na majonzi? Mzee wangu umeshindwa kuandika hata mstari mmoja tu wa rambi rambi kwa wazanzibari?

Chakula ni nini kwa mwanadamu? Hao waliokwenda na maji wameacha vyakula vingapi? Na ina maana kabla ya CCM kupeleka huo wali wa shughuli huko Igunga wananchi wa Igunga walikuwa wanakufa njaa? Walikuwa hawali chakula? Hawapiki majumbani mwao? Hivi kumbe chakula ndivyo kilivyo na thamani hivi kwenu? Ndio maana kwenye shughuli zenu watu hawaji mpaka wawe na kadi na watoe pesa kwa sababu mnaogopa watakula?

Je umefanya utafiti ukajua kuwa hicho chakula kilichopigwa picha kilikuwa kwa ajili ya kina nani? Yaani kimantiki inaingia akilini kweli hizo sinia chache kilishe maelfu ya wananchi wa Igunga waliohudhuria uzinduzi siku hiyo? Mimi si msomi wala mwana CCM lakini kwa akili ya kawaida na shughuli za uswahilini ninavyozifahamu kutokana na kazi zangu za jamii, hicho chakula kitakuwa kiliandaliwa kwa ajili ya makundi ya wasanii waliokwenda kutumbuiza hapo uwanjani na wageni wengine na kitakuwa kimeandaliwa na wenyeji wa Igunga kupitia chama chao.

Wakati mwingine mjaribu basi hata kuangalia mantiki ya tukio au picha kabla hamjaitafsiri na kuwatukana wenyeji wa eneo hilo kwa kuwa tu watu hao hawana uwezo wa kuingia humu na kujitetea au kusema ukweli. Chakula/wali/ubwabwa, mnakithamini sana hata mmeshindwa kuchangia wenye njaa huko East Afrika hata kupitia kwa Mjengwablog kwa hofu kuwa watu watakula! Umenifanya kweli nifikirie mara mbili mbili sijui umeteleza au umedhamiria. By the way nimefanya kazi kwenye jamii miaka mingi sana na ninachukia sana mitazamo ya wasomi kuwaona kuwa watu masikini wa vijijini ni irrationa and cannot make rational decision. Nitarudi tena nikwambie kwanini maeneo hayo CCM wanashinda very simple haihitaji kufanya Logarithms au Aljebra!!

Mbele said...

Anonymous, mimi ndiye mwamuzi wa nini cha kuweka au kutokuweka katika blogu yangu.

Pamoja na hayo, siingilii uhuru wa wasomaji wanaochangia.

Nimewahi kuandika makala nikielezea kwa nini ninablogu, na humo nimeelezea kuwa blogu yangu ni sehemu binafsi ambapo naweka chochote nitakacho, kuanzia kumbukumbu, mawazo, hisia, na kadhalika.

Kama unavyoona, hii habari ya wali sijaiwekea uchambuzi wowote. Hayo unayosema na masuali unayouliza hayanihusu.

Suala la maafa ya Taifa linatugusa sote. Unavyojaribu kujenga hisia kuwa wengine hawalioni suala hili unavuka mpaka na huna ushahidi.

Kuna namna nyingi za kujumuika na waathirika katika majanga. Kuandika rambirambi katika blogu ni namna moja tu, wala usiiongelea kama vile ni ya pekee sana.

Nikitumia mantiki yako mwenyewe, kuwa wengi hawana uwezo wa kuingia katika blogu, ukumbuke kuwa wengi wa waathirika wa janga hili la sasa nao hawaingii kwenye blogu.

Kwa maana hiyo, kuwakumbuka katika sala huenda ni njia muafaka zaidi ya kuungana nao, kwani mwenye uwezo juu ya yote ni Mungu. Na kwa mujibu wa mafundisho ya dini, inatosha ukifanya mambo hayo kimya kimya.

Vile vile, suala la kuchangia pesa majanga haya sio suala ambalo limepangiwa muda, kwamba kesho au keshokutwa itakuwa mwisho. Wanaotaka kutoa michango ya fedha kwa majanga haya wanayo fursa ya kuendelea kutoa. Usiwanyooshee watu vidole kwa vile tu majina yao hayaonekani Mjengwablog.

haliembe said...

songa mbele baba hao ndio wanaoiangamiza tz kwani hali ni mbaya sana kuweka au kuondoa kitu chochote katika blog yako ni haki yako binafsi

Anonymous said...

"Nikitumia mantiki yako mwenyewe, kuwa wengi hawana uwezo wa kuingia katika blogu, ukumbuke kuwa wengi wa waathirika wa janga hili la sasa nao hawaingii kwenye blogu."

Nimekunukuu ili nipate kukujibu kwenye hicho kipengele tu. Hivi unafikiri waliotharika na janga la kuzama kwa meli ni wale waliofariki kwenye hiyo ajali tu ambao hawaingii kwenye hii blogu kwa kuwa wamekufa?

Au wale majeruhi waliopo hospitali hawaingii kwenye blogu yako kwa kuwa ni masikini wa kutupwa? Na kwa kuwa hawaingii kwenye blogu yako basi haina haja wala maana kuwapa pole ndugu na jamaa zao?

Au unafikiri walioathirika na hilo janga ni makundi hayo mawili tu na si ndugu na jamaa zao ambao nao wameathirika kwa kufiwa na ndugu zao au kuuguza ndugu zao walionusurika na hiyo ajali?

Ngoja nikwambie almost every household Unguja na Pemba kuna msiba, na nyumba nyingine zimepoteza mtu zaidi ya mmoja. Na hata mie ninavyoandika hapa nimepoteza ndugu katika ajali hiyo. Kila Mpemba au Muunguja amepoteza ama ndugu wa karibu sana au ndugu wa kuoleana au jamaa katika ajali hiyo.

Sikukulazimisha uwape pole na wewe ndiye mwenye mamlaka na maamuzi ya mwisho kuwafariji watu waliofilia, lakini kwa kuwa unaona kuwa hawana uwezo wa kuingia kwenye blogu yako na hayakuhusu yote ni sawa tu. Kwani katika jamii yetu wenye mtazamo kama wako ni wengi tu, mifano hai tumeiona huko Bara kwani hata TBC1 walishindwa kutangaza habari hizi kutwa nzima tena ndilo shirika la serikali sembuse wewe mwenye blogu yako binafsi?

Yanakuhusu nini mambo ya watu wasiotembelea blogu yako na wasio na faida na wewe ati. Haya bwana mkubwa baki na blogu yako na sie masikini wacha tuache kukufuata kwenye blogu yako.

Anonymous said...

Ugomvi wa nini? Kama mtu hajisikii kuandika habari za msiba unamlazimisha wa nini? Yesu aliwahi kusema: waache wafu wazike wafu wenzao. Kufa ni kitu cha kawaida lakini kutoa rushwa tena kwa kuuza haki za walio hai si jambo la kupuuzia. Wazanzibari acheni unafiki na kujipenda sana. Mnapochoma mabaa mbona hamlaumu wasiochapisha habari hiyo? Kufa hakufurahishi lakini mzee Mbele angefanya nini iwapo wanaohongwa wali ndiyo hao hao wanaosababisha kuwapo serikali mbovu zinazochangia kutokea kwa maafa hayo? Nadhani ananymous ameshindwa kupambanua mambo mepesi.
Usitumie mihasira ya kufiwa hao wenzio kuwahukumu wenzako. Kama mtanzania yeyote, vifo vitokanavyo na uzembe vitaongezeka iwapo hatutakata mzizi ambao ni serikali haramu zikiongozwa na watawala haramu ambao wakiguswa mnakimbilia kusema wanasemwa kwa vile ni waislam. Mbona mnashindwa kuwashutumu kwa uzembe uliosababisha vifo vya wapendwa wenu au kwa vile ni waislam?

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...