Sunday, September 25, 2011

Hotuba ya Rais Mugabe, Kikao cha 66 cha Umoja wa Mataifa

Hotuba hii imenigusa. Inanikumbusha enzi za Mwalimu Nyerere, ambapo alikuwa anapambana na hao wakoloni mamboleo ambao leo sisi wa-Tanzania, kwa kukosa mwelekeo na fikra thabiti, tunawaenzi kama marafiki na wadau wa maendeleo yetu.


4 comments:

Simon Kitururu said...

Rais Mugabe akiongelea wengine mara nyingi huwa ananigusa sana !

Tatizo liko kwenye vitendo vyake afanyavyo mwenyewe kama kiongozi pia ambavyo sina uhakika navyo sana kikuvikubali hasa vya miaka hii ya karibuni!:-(

Anonymous said...

kama kawaida ya marais wa afrika, wakiongelea mambo ya wnengone ni wazuri sana na ukizubaa, unaweza kulia, vp ghadaf na umoja wa afrika? njoo kwenye ishu zao ndani ya nchi;HATARI

Simon Kitururu said...

@Anony: Nasikia kunawadaio hata OBAMA kaambukizwa GENE ya kuongea sana bila vitendo!:-(

tz biashara said...

Hakuna binaadamu aliekamilika lazima unakuwa na kasoro.Kumbukeni Zimbamwe ya zamani ilikuwa ni nzuri sana kiuchumi na kila kitu.Lakini wenzetu wa magharibi wakiamua kukupamba basi watakupamba ilimradi uwafate vile wanavotaka,lakini ukiwakaidi basi wanayonjia ya kukupaka matope na uchukiwe na wengi.

Mugabe huyu akiondoka basi nchi itakuwa chini ya wa magharibi.Nauhakika kuna watu wanaiendesha nchi ya Zimbabwe na ndio chaguo lao Mugabe maana hamuogopi mtu yeyote na anauwezo wa kumwambia kitu chochote.Na ndio maana anaweza kuwaambia ukweli bila ya uoga.Tofauti na Raisi wetu aliongea vizuri lakini kuna mambo kama ya Libya aliogopa kuelezea.

Wa magharibi bado wanataka kuendeleza ukoloni na hasa ukitizama uchumi wao hivi sasa ni mbaya sana ambao umechangiwa na vita wanayopigana kila kona na yote haya wanataka kuendelea kutawala dunia na ni kitu hakiwezekani.

Watu wa zamani hawakusoma lakini sasa hivi wengi wamesoma na historia hujirudia siku zote.

Mugabe anaendesha nchi kiubabe kwa sababu wa magharibi wanataka kuinyonya nchi ya waafrika na ndio maana kaamua kumbana mpinzani wake kwasababu alikuwa kibaraka wa wazungu.Uchumi wa Zimbabwe umekufa kwasababu ya kuwekewa vikwazo na wamagharibi.

Wamagharibi kazi yao ni kuua tu na ni kama fun yao au kama wanacheza gemu ktk computer.Waafrika au wa Asia wamekuwa hawana thamani ktk dunia hii isipokuwa wao tu ndio muhimu ktk dunia hii.

well done Mugabe.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...