Friday, September 16, 2011

Nimetua Indianapolis

Nimerejea kutoka Tanzania tarehe 6 mwezi huu, na tayari nimeshaanza mizunguko. Leo alasiri nimetua Indianapolis, Indiana, kuhudhuria mkutano wa Africa Network, mtandao wa vyuo vya hapa Marekani ambao lengo lake ni kuhamasisha na kuendeleza masomo yahusuyo Afrika. Tunajenga mikakati ya ushirikiano katika utafiti, ufundishaji, na kubadilishana uzoefu wa aina mbali mbali. Hatimaye tunataka kuendeleza ushirikiano baina ya vyuo vyetu hivi na vyuo vya Afrika, kwa mfano kwa kupeleka wanafunzi na watafiti Afrika na kupokea wanafunzi na watafiti kutoka Afrika.

Nimekuwa mwanabodi wa bodi ya Africa Network tangu ilipoanza, miaka mitano iliyopita. Ni shughuli ya kujitolea, lakini napenda shughuli za aina hiyo. Kuna mambo mengi yanayonivutia katika mikutano yetu, kwa mfano kukutana na walimu ambao wanaandaa programu za kupeleka wanafunzi Afrika na kuwapa ushauri na mawaidha.

3 comments:

Unknown said...

Hongera sana Prof.

Anonymous said...

hongera sana mzee

Mbele said...

Shukrani wadau. Ni masuala ya kuwatengenezea fursa watafiti na wanafunzi, hapa Marekani na Afrika, na pia sisi wenyewe kujiongezea fursa ya mawasiliano na ushirikiano na wengine.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...