Tuesday, May 15, 2012

Burudani Longido

Hapa kushoto ni mpiga gitaa tuliyemkuta Longido mwaka 2008. Longido ni mji mdogo kwenye barabara itokayo Arusha kwenda Namanga. Ni karibu na Namanga. Nilikuwa hapo na wanafunzi katika kozi kuhusu mwandishi Hemingway.
Tulikaa hapo siku mbili, tukifuatilia habari za Hemingway, ambaye alikuwa Kenya na Tanganyika miaka ya 1933-34 na 1953-54, akaandika mambo kadhaa kutokana na kuwepo kwake pande hizi. Hapo Longido tulikuwa wageni wa programu ya utalii inayoendeshwa na wenyeji wa hapo.
Akina mama walitupikia vizuri na baada ya chakula cha jioni ilifuata burudani ya muziki.
Huyu ndugu alikuwa anapiga gitaa na kuimba nyimbo mbali mbali, zikiwemo "zilipendwa" za Afrika Mashariki na za Marekani. Tulifurahi sana kwa burudani hiyo.

2 comments:

emuthree said...

2008,....mmh, leo 2012. Twashukuru Profesa, kwa kumbukumbu hii, tupo pamoja!

Mbele said...

Shukrani, emu-three, kwa ujumbe wako wa mshikamano. Jana, mwanafunzi mmoja aliyekuja kwenye hii kozi kaniandikia kule Facebook akisema kuwa ana kumbukumbu nzuri za safari yetu ile, na anatamani kuja tena Tanzania. Nami bila kuchelewa nimemkaribisha vilivyo, kwa niaba yenu waBongo wenzangu.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...