Sunday, May 6, 2012

Mama Mjasiriamali, Baina ya Matema Beach na Tukuyu

Mwaka jana, nilifika hadi mkoani Mbeya, nikiwa na wanafunzi kutoka Marekani, kama nilivyoelezea hapa. Tukiwa njiani kutoka Matema Beach kuelekea Tukuyu, tulimkuta mama anauza soda na bidhaa zingine katika kibanda kando ya barabara. Mama huyu anaonekana hapa kushoto kabisa.







Tulisimama hapo na kununua vitu viwili vitatu.
Kila ninapomkumbuka mama yule najiwa na mawazo ambayo yalinijia siku ile. Ni kuhusu wajasiriamali wanawake. Nimesoma taarifa kuwa akina mama hao wenye kipato hafifu wakiwezeshwa, huwa wajasiriamali makini. Mama kama huyu akipata mtaji mkubwa anaweza kufanya mambo makubwa.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli kabisa. Nampongeza sana kwa utundu wake. Inasikitisha pale watu wanaposema wanawake hawawezi, si wabunifu. Lakini wanawake TUNAWEZA.

Mbele said...

Ukifuatilia, unaweza kukuta kuwa mama kama huyu anaanga bajeti kwa uangalifu sana, ananunua mahitaji ya nyumbani, anasomesha watoto, na kadhalika.

Taarifa nilizogusia zinasema kuwa popote katika hii dunia inayoitwa "ya tatu" akina mama wakikopeshwa mitaji hurejesha ipasavyo.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...