Wednesday, May 30, 2012

Warembo Wengine Hawa Hapa

Siku chache zilizopita, niliweka makala kuhusu mrembo hapa katika blogu yangu. Lengo langu lilikuwa kuchochea mjadala kuhusu suala la urembo, ambalo, kama nilivyogusia, nimelijadili katika kitabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences.

Nimeona picha nyingine ya warembo katika mtandao wa Facebook, ambayo naileta hapa. Sisi tuliokulia vijijini Afrika tunaweza kusema kuwa ingekuwa bora kama hao warembo wangejisitiri vizuri zaidi kimavazi. Lakini huenda hao si wa-Afrika. Hapa Marekani, kwa mfano, wakati wa joto, watu wengi huvaa vivazi ambavyo kwetu tunaviona si vya heshima, lakini hapa wanaona ni sawa.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nakubaliana na Prof. Hata mimi pamoja na kuwa ni mwanamke lakini huwa nasumbuliwa sana na vivazi kama hivyo. Labda ni kweli kwa vile tumekulia kijijini.

Mbele said...

Dada Yasinta, shukrani kwa ujumbe wako.

Kwa vile nimetaja mambo ya hapa ughaibuni, napenda kuongezea kwamba shughuli yangu mojawapo ni kuwaandaa wanafunzi wa ki-Marekani wanaoenda kusoma kwa muda kwenye vyuo vya Afrika, kama vile Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Katika kuwaandaa, suala la kuwaelimisha kuhudu tofauti za tamaduni ni muhimu, na ilikuwa ni shughuli hii ndio iliyonifanya nikaandika kitabu nilichokitaja hapa juu, ambacho wengine nao wananikitumia.

Inapokuja kwenye suala la mavazi, nawapa msisitizo wanafunzi wa kike kuwa kule kwetu, haifai kabisa kuvaa vivazi wanavyovaa hapa wakati wa joto, ambavyo baadhi ni kama vichupi. Nawaambia kwamba ni vema wakaviacha hapa hapa Marekani.

Na kweli, ninapozunguka na hao wanafunzi huko mikoani, wanajionea wenyewe jinsi wanawake wanavyovaa. Nimezunguka nao sehemu kama Iringa, Mbeya, Karatu, Babati, Longido, Namanga, Mto wa Mbu, na kote huko wanajionea mavazi tunayoyaita ya heshima. Ni wajibu nao wavae kwa namna inayokubalika kwenye nchi husika.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...