Monday, May 7, 2012

Kituoni Mbamba Bay

Hapa ni eneo la kituo cha mabasi Mbamba Bay. Kama hakuna basi, unachoona ni huu uwanja na maduka pembeni, Nilikuwepo Mbamba Bay mwaka jana, kama nilivyoelezea hapa. Picha zinazoonekana hapa nilipiga wakati huo. Upande wa kulia wa mlima unaoonekana ndipo ziwani.
Maduka yameuzunguka uwanja huu, kama nilivyogusia hapa. Nyumba inayoonekana kulia katika picha hii hapa ndio ofisi ya kukatia tiketi. Kwa vile mji ni mdogo sana, na mabasi ni labda mawili tu kwa siku, ofisi haina kazi nyingi kama ilivyo katika miji mikubwa.
Basi likishafika, uwanja huu unapata uhai, kwa maana ya kuwepo na watu wengi, wakiwemo wasafiri wanaoshuka na wengine wanaopanda basi. Basi hili lilikuwa linatoka Liuli, likiwa njiani kwenda Songea.

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Duh! unanikumbusha mengi sana maana mwaka jana sikufika mpaka huko niliishia Songea /Ruhuwiko tu. Faida kubwa sana hii katika kumbukumbu.

Mbele said...

Ninazo picha zaidi za Mbamba Bay. Insh'Allah nitaziweka hapa kijiweni pangu. Najua kuwa hakuna anayeweza kuzitembelea sehemu zote za nchi yetu. Kwa hivi picha zinasaidia.

Yasinta Ngonyani said...

kweli kabisa nami ngoja niweke za huko ingawa za zamani kiduchu..

Unknown said...

Hilo basi la Kangaulaya linatoka liuli vikapu vikiwa vinaning'ia?,hlo lazma linaenda liuli kwakuwa vikapu huwa vnarudi vitupu toka Songea!

Mbele said...

Ndugu Matembo, shukrani kwa ufafanuzi. Umenipa mwanga, na naamini wadau wengine nao wamefaidika.