Saturday, January 10, 2015

Tumefanya Kikao cha Bodi ya "Africa Network"

Leo tulikuwa na kikao cha bodi ya Africa Network. Hii jumuia ya vyuo vya Marekani ambavyo vinataka kushirikiana katika ufundishaji na utafiti kuhusu Afrika. Mwanzilishi wake ni Profesa Tom Benson.

Kikao chetu cha leo kilikuwa cha kutumia simu ("teleconferencing"). Hii ni tekinolojia ambayo haihitaji watu kusafiri na kukutana uso kwa uso. Nimeshiriki mikutano ya aina hii mara nyingi katika nyadhifa zangu kama mwanabodi wa Africa Network na Afrifest.

Leo tumeongelea zaidi masuala ya kutafuta fedha, kuboresha tovuti yetu, na kupata wanachama wengine. Mbali na suala la tovuti yetu, tumeongelea pia suala pana zaidi la kujiingiza katika mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter.

Jambo jingine muhimu ambalo tumekubaliana ni kuwa badala ya kuwa na mkutano wa jumuia yote mwaka huu, tufanye kikao cha wanabodi pekee, ili kujinoa katika masuala mbali ya uendeshaji wa Africa Network na kujipanga kwa miaka ijayo. Tutafanya kikao hiki mwezi Aprili, mjini Chicago.

No comments: