Tuesday, July 14, 2015

Nawashangaa CCM

Ninawashangaa wanaCCM wanaolalamikia mchakato wa chama chao wa kumpata mgombea urais. Mwaka 2010 CHADEMA walilalamika sana kwamba wamefanyiwa rafu na CCM. Hakuna yeyote katika CCM aliyewasikiliza CHADEMA, wala kuwaonea huruma. CCM wote waliibeza CHADEMA, kwamba ingojee uchaguzi ujao.

Sasa leo wanalalamika kuwa wamefanyiwa rafu huko huko CCM. Sio kwamba hao wanachukia rafu. Wanalalamika kwa sababu rafu wamefanyiwa wao. Mimi kama raia ambaye si mwanachama wa chama chochote cha siasa naona kuwa hawana sababu ya kulalamika, kwani wanavuna walichopanda. Labda watajifunza umuhimu wa kutetea haki wakati wote na kwa yeyote.

1 comment:

Mbele said...

Inaonekana suala hili ni pana. Kingunge Ngombale Mwiru ameongelea mchakato katika CCM wa kumchagua mgombea urais. Soma taarifa hii.