Monday, September 28, 2015

Kampeni za CCM Mwaka Huu

Najaribu kutafakari picha hii iliyopigwa katika moja ya mikutano ya kampeni za uchaguzi zinazoendelea Tanzania. Ina maana kwamba mwenye uwezo wa kupiga "push-up" nyingi ndio anafaa kuwa kiongozi? Je, ili uukwae ubunge, unatakiwa upige angalau "push-up" ngapi? Udiwani je? Na ili uwe waziri, unahitaji "push-up" ngapi? Na kwa uwaziri, ni sahihi tuwe na "push-up" tu au na kuruka viunzi pia? Na kwa kuzingatia uzito wa cheo cha uwaziri, kwa nini tusiongezee pia uwezo wa kunyanyua matofali angalau manne ya zege? Kwa kweli, tukifanya hivyo, tutapata serikali imara kabisa.

1 comment:

PBF Rungwe Pilot Project said...

Niionavyo mimi ni kwamba hakuwa uhusiano wa uwezo wa kupiga push up na uwezo wa kuongoza watu.Kama kigezo ni hicho wainua vitu vizito wangekuwa ndiyo viongozi wetu ama wangepaswa wawe ndiyo wa kuchaguliwa.