Saturday, January 14, 2012

Januari 16, Kumbukumbu ya Martin Luther King,Tukutane St. Paul

Tarehe 16 Januari ni kumbukumbu ya Martin Luther King hapa Marekani. Zitafanyika shamrashamra nyingi sehemu mbali mbali. Kwenye miji kama Minneapolis na St. Paul, Minnesota, itakuwa vigumu hata kuamua wapi kwa kwenda.

Lakini mimi nilishajisajili kama mshiriki wa maonesho yatakayofanyika Chuoni Concordia, mjini St. Paul. Pamoja na waandishi wengine, tutakuwa pale na vitabu vyetu, tukikutana na wadau na kubadilishana mawazo, kuanzia saa 3:30 asubuhi hadi saa 9 alasiri.

Nafurahi kwamba miaka ya karibuni nimefanya juhudi ya kusoma habari za Martin Luther King na baadhi ya maandishi yake, hadi kufahamu jinsi alivyothamini elimu, sawa na Mwalimu Nyerere, na jinsi alivyotufundisha kujali usawa na haki za binadamu wote. Wala hakuwa upande wa watu weusi tu, kama wengi wanavyoamini.

Nimegundua kuwa wengi, hata hao wa-Marekani Weusi ambao wanapenda sana kumtaja na kumpigia mfano, hawamwelewi vizuri Martin Luther King. Nangojea kwa hamu kubadilishana mawazo na hata kulumbana na umati wa watu watakaohudhuria hiyo maadhimisho hiyo tareye 16 Januari. Karibuni.

2 comments:

Subi Nukta said...

Profesa Mbele naomba kutoka nje ya mada na hii ni kutokana na 'coincidence' iliyotokea. Nimemaliza kusoma taarifa ya kina kuhusu ile meli ya Concordia iliyozama huko Giglio, Italia, kisha nikafungua taarifa ya pili ndiyo habari toka kwenye blogu yako, nikajuliza, he! hii Concordia aliyoiandika Prof. hapa ndiyo ile ya ajali au hii ni nyingine? Ikanibidi nifike hapa kusoma post nzima ndiyo nimegundua ni majina tu yamefanana, mada na matukio ni tofauti kabisa.

Haya, uwe salama huko Concordia kusherehekea sikukuu ya kumbukumbu ya MLK.

Mbele said...

Da Subi, shukrani kwa ujumbe wako. Sikuwa nimesikia bado kuhusu kuzama kwa hii meli iitwayo Concordia. Ndio nimeisikia kutoka kwako, halafu nikaenda mtandaoni kufuatilia.

Hapa Minnesota penyewe pana vyuo viwili vyenye jina hilo hilo la Concordia. Kuna Concordia College (ambayo iko kwenye mji wa Moorhead), na Concordia University (ambayo iko mjini St. Paul). Halafu Canada pia kuna chuo kikuu kiitwacho Concordia. Ni rahisi kujichanganya na kuvichanganya.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...