Video hii imenisisimua akili. Sikujua kuwa maandamano ni mpango wa makafiri na kwamba hakuna maandamano katika u-Islam
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
3 comments:
Kwakweli mimi binafsi sijui kiarabu japokuwa neno moja moja naweza kulipata kutokana na kugha ya kiarabu haipo mbali sana na kiswahili.
Uisilamu unakataza mambo mabaya na unakubali mambo mazuri.Unakataza uonevu na unyanyasaji na unataka haki kwa kila mmoja awe tajiri au masikini na hata awe kiongozi mdogo au mkubwa.
Na maandamano ni mkusanyiko wa watu walioungana kupinga au kukubali jambo.Sasa hutegemea jambo lipi linalosapotiwa au kupingwa na waandamanaji hao.
Kama kutakuwa na watu wanaandamana kwa kupinga jambo linalokubalika kiisilamu basi haiwezi kuitwa uchochezi hata siku moja.Kitu kitakachokubalika ktk uisilamu ni kile ambacho kinanidhamu ya kudai haki ambayo inaweza kuwa inafanana na maandamano yaliyotokea majuzi kwetu.
Kwasababu sisi waisilamu tunaifuata Quraan na sijawahi kuona hata sehemu iliyoandikwa kutokubalika kwa maandamano,basi siwezi kukubaliana na huyu shekhe.Au inawezekana hiyo clip haijachukuliwa yote tukaweza kuijadili topic nzima ambayo aliyoikusudia huyu sheikh na inawezekana alikusudia maandamano yakuchochea madhambi tu lakini sio ya kudai haki.
Uisilamu unahimiza kutenda haki na kama kutakosekana haki basi inatakiwa kuidai haki hiyo kwakuwa ni haki yako.Na kama hatutadai haki inamaana tuiache serikali ifanye inavotaka huku wananchi wananyanyaswa na kuwa masikini wakati viongozi na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya wanajiongezea utajiri.
Maandamano yanasaidia kupunguza kasi ya uonevu kwa kiasi fulani na yanasaidia kuwakumbusha waonevu kujirekebisha kwa kuwa watu wanaona na wanajua wanachofanya.
Kama waisilamu tungekuwa haturuhusiwi kuandamana basi waarabu (Arab springs) wasingeandamana kwasababu maandamano yao yanasapotiwa hata na mashekhe wakubwa waliosomea dini vizuri sana.
Naomba Profesa sikiliza huyu sheikh Yusuf aivoitafsiri uisilamu.
http://www.youtube.com/watch?v=AD2EgGG5iUQ&feature=related
Shukrani sana tz biashara, kwa maoni na mawaidha yako. Napenda niseme kuwa daima nafarijika na kushukuru ninaposoma unayoandika. Unalenga kwenye hoja na unaheshimu mawazo ya wengine, hata kama hukubaliani nayo. Umetanguliza heshima. Mungu akubariki, uendelee kutoa mchango wako.
Ingekuwa wa-Islam wote na wa-Kristu wote wana moyo na mwelekeo kama wako, hatungekuwa na haya matatizo mengi tunayoyaona.
Nikirudi kwenye kauli ya huyu shekhe, nami nimekuwa nikiwazia alitoa kauli hii katika mazingira yepi. Na hilo nawe umeligusia. Tuko pamoja.
Nimeangalia mtandaoni, na bado naangalia, ili nipata jibu. Ni njia mojawapo ya kumtendea haki, kwa maana kwamba maneno yake yasinyofolewe kutoka kwenye mkabala husika.
Lazima nikiri pia kuwa nilieta ujumbe ule kama kauchokozi fulani pia. Mimi ni mwalimu wa vyuo vikuu, na mazoea ya darasani ya kutoa mawazo kiuchokozi, ili kuwachemsha vichwa wanafunzi, ni mazoea ambayo ni vigumu kuondokana nayo ninapokuwa uraiani. Hizi blogu ni sehemu muhimu ya uraiani.
Shukrani kwa kunipa "linki" ya video. Nitaenda kuisikiliza.
Mungu akubariki, kwa moyo wako wa kulenga katika kusikilizana, kuelewana na kuelimishana.
Post a Comment