Sunday, January 22, 2012

Naikumbuka Matema Beach

Tanzania ina sehemu nyingi zinazopendeza sana, nami nimebahatika kuziona baadhi ya sehemu hizo. Mwaka jana, kwa mfano, nilipata bahati ya kufika Matema Beach, pwani ya kaskazini ya Ziwa Nyasa. Ni sehemu nzuri sana kwa mapumziko. Imetulia na haina msongamano na misuguano kama ya Dar es Salaam. Hapa kushoto naonekana nimetulia kwenye bembea, nikifaidi upepo mwanana. Huyu binti ni mmoja wa wanafunzi wawili niliowaleta hapo kwenye ziara ya kuifahamu nchi.

Ukifika ufukweni hapo, unaweza kujikalia mahali chini ya mti, unapiga mbonji, kama wasemavyo watoto wa vijiweni, au ukawa unasoma kitabu, kupiga michapo na wenyeji, au kuangalia Ziwa na mitumbwi ipitayo humo.

NImeandika mara kadhaa kuhusu Matema Beach katika blogu zangu, kwa mfano hapa na hapa, na napangia kuendelea kuandika.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

hata mia naikumbuka sana bahati mbaya tulikuwa huko tofauti mwaka jana...ni sehemu nzuri sana asiyefika basi na ajaribu kufika:-)

Mbele said...

Nakumbuka sana kuwa uliwahi kutuambia kuwa ulifika hapa Matema. Nina hamu ya kuona picha zako, kama ulipiga.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...