Sunday, February 26, 2012

Mapinduzi Bora Nyumbani

3 comments:

tz biashara said...

Mambo ni kusaidiana profesa.Na mtoto anaelelewa ktk nyumba yenye nidhamu basi siku zote mtoto atakuwa na nidhamu.Anapokuwa na kuona baba na mama walikuwa wanaishi kama timu ambayo wanashirikiana majukumu ya ndani na nje,basi na mtoto atakuwa hodari kwa mengi kwasababu amepata mapenzi na mafunzo kwao.Na mtoto akilelewa ktk nyumba isio na nidhamu,ulevi,ugomvi na hata wizi basi mtoto ndivo atakavokuwa na hizo tabia.Kwasababu akimuona baba karudi kalewa na anampiga mama yake na yeye atakapokuwa mkubwa atafanya hivo kwa mama watoto wake.

Naamini kwamba jamii nzuri hutengenezwa na mzazi kwanza.Na elimu bora vilevile inachangiwa na mzazi.Kwasababu mzazi akijishirikisha kwa mtoto ktk elimu kwa kumsaidia home work au hata kukaa nae kujaribu kusoma nae kitabu au kufanya challenge za marthematics humsaidia mtoto kwa kiasi kikubwa.Lakini wazazi wengi hufikiria jukumu la elimu ni la mwalimu na mwanafunzi mwenyewe.

Mbele said...

Kuna manufaa sana mwanamme unapolea mtoto mchanga. Wakati nasoma hapa Marekani, tulipata mtoto, kwa njia ya operesheni, ikabidi mama apumzike kabisa kwa miezi mitatu.

Manesi walinikabidhi mtoto akiwa na wiki moja, wakanielekeza namna ya kumtunza kwa kila hali. Kwa miezi yote hiyo nilifanya kila anachofanya mama mtoto, ukiachilia mbali kumnyonyesha kwa maziwa yake. Hicho tu ambacho sikuweza, bali nilikuwa namnyonyesha maziwa ya dukani.

Matokeo yake ni kwamba mtoto alinizoea na kunipenda mimi, sawa na watoto wanavyomzoea mama. Kusema kweli, nawasikitikia wanaume wa kwetu wanavyojikosesha raha ya kupendwa na mtoto ambayo niliipata mimi. Tuliendelea kukaa Marekani kwa miaka mitatu zaidi hadi nikamaliza masomo, na muda wote huyu mtoto alikuwa sambamba na mimi kama vile mama yake.

Hata tulipofika Tanzania, mwaka 1986, hali ilikuwa hiyo. Mtoto akihitaji chochote, kama vile kwenda bafuni, ananikimbilia mimi, na mimi nakimbia kwenda kumtimizia anachohitaji. Watu walikuwa wananishanga.

Jambo jingine ni kuwa kuanzia pale, mimi sithubutu kuwalaumu akina mama wenye watoto wanapochelewa katika kujiandaa kwenda popote.

Utawasikia wanaume wanalalamika kuwa wanawake wanachelewesha safari, mara hili mara lile. Mimi ambaye nilishayaona mambo ya kumwandaa mtoto, halafu unapotoka naye nje ukawahi basi, ugundue kuwa umesahau labda chupa yake ya maziwa, au poda, au mtoto amejisaidia na lazima urudi ukaanze upya, sithubutu kuwalaumu wanawake. Mtoto anahitaji mambo mengi na kuyashughulikia yote inahitaji muda. Na kuchelewa ni lazima.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Tulioko huku ughaibuni tumelishalizoea hili. Na uhusiano unaojengeka kati ya baba na mwana ni imara ajabu (wa baba na mkewe huo siusemei...)

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...