Hapa ni mjini Faribault, Minnesota, wakati wa tamasha la tamaduni mbali mbali.
Hapa ni Sinza, Dar es Salaam. Huyu mdau ni Gilbert Mahenge, mwanakijiji wa Msoga, Bagamoyo. Huyu ni kati ya wa-Tanzania wachache ambao nawaona wameelimika kiukweli, kwa maana kwamba anatafuta elimu bila kuchoka. Mara ya kwanza kukutana naye, tulikuwa kwenye basi tukitokea Dar es Salaam. Katika begi lake alikuwa na vitabu. Hapo Sinza pia, tulipokutana tena, alikuwa na vitabu, hata akaniulizia kuhusu kitabu fulani ambacho sikuwa nimekisikia. Yeye alishakisoma. Hasomi kwa sababu ya mitihani, bali kwa kujielimisha.
Hiyo ni familia ya ki-Jerumani. Tulipiga picha hii kituo cha mabasi Ubungo, Dar es Salaam, wakati wao walipokuwa wanasafiri kwenda Ruvuma, ambako alizaliwa huyu mama wa familia, aliye pembeni yangu.
Hapa ni Brooklyn Park, Minnesota, kwenye tamasha la nchi za ki-Afrika. Huyu wa katikati ni mdau Richard Fillie kuoka Sierra Leone. Alimleta huyu mwingine, ambaye anatoka Sudan. Staili yao ya kushika vitabu ni tofauti na ya wengine.
Hapa ni viwanja vya makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam, Septemba, 2004, wakati wa tamasha la vitabu. Niko na dada yangu na mdau Eiko Kimura kutoka Japani.
Hapa ni Minneapolis, Minnesota, kwenye mkutano wa watu wenye asili ya Afrika. Huyu mdau naye ni mwandishi M. Ann Pritchard.
Hapa ni viwanja vya makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam, Septemba, 2004, wakati wa tamasha la vitabu. Niko na mdau kutoka Japani. Yeye amevisogeza vitabu karibu na kifua changu.
No comments:
Post a Comment