Wednesday, February 15, 2012

Maskat: Mbunifu wa Mitindo

Katika pita pita zangu mtandaoni, nilikumbana na taarifa kwenye blogu ya Swahili na Waswahili kuhusu mwanamitindo Maskat, m-Tanzania ambaye jina lake jingine ni Hayakuhusu. Nilivutiwa na taarifa hiyo, nikaifuatiliza zaidi, nikaona jinsi dada huyu alivyo mjasiriamali makini.













Sio tu anajibidisha katika fani hii ya mitindo, bali anazitumia vilivyo tekinolojia za mawasiliano ya kisasa. Utamkuta sehemu kama Youtube, Facebook na blogu yake. Anwani yake ni maskatdehaan@hotmail.com. Napenda kusoma habari za watu wa aina hii na pia kuzitangaza katika blogu yangu, kwani ni changamoto kwa wengine, hasa watoto na vjiana wetu. Wanasema kuwa picha inajeleza sawa na maneno elfu. Kwa kuangalia picha za Dada Maskat, napata hisia kuwa ni dada anayejipenda na kujiamini, anayejua anachofanya na anakoelekea. Hili ni fundisho muhimu kwa watoto wetu, na sisi wenye mabinti tuna sababu ya ziada ya kuuenzi mfano wa dada Maskat.

2 comments:

Rachel Siwa said...

Ubarikiwe sana kaka Mbele kwa Moyo wa kusaidia.Na maneno/Ushauri wako nimejifunza sana kupia wewe,Pamoja sana.

Mbele said...

Dada Rachel, kwanza nikushukuru wewe, kwa vile niliona taarifa hii kwa mara ya kwenye blogu yako.

Inafariji na inafurahisha kujumuika na wengine katika kuhamasisha na kutangaza mambo mema na mazuri maishani, mambo yanayojenga, sio kubomoa. Baraka tele zinatuteremkia tunapofanya hivyo. Hilo naliamini kabisa. Tuko pamoja.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...