Katika mizunguko yangu mwaka jana nchini Tanzania, pamoja na wanafunzi wangu wawili, nilikaa siku kadhaa mjini Iringa. Hapo nilimtafuta Mwenyekiti Mjengwa, mmiliki na mwendeshaji wa Mjengwablog. Tulienda ofisini kwake katika Akiba House. Tulikaribishwa vizuri, tukaelezwa shughuli za ofisi hii.
Hatukukaa sana hapa ofisini. Tuliulizia mahali pa kupata chakula cha mchana na Mwenyekiti akatupeleka Neema Craft. Tulipata fursa ya kuongea naye kuhusu mambo kadhaa, yakiwemo ya utaratibu wa vyuo vingi vya Marekani wa kupeleka wanafunzi kwenye masomo nchi za nje na pia kuhusu mawasiliano ya kijamii kama vile blogu. Baada ya hapo tulipanda dala dala tukaenda Kalenga. Natumia dala dala kwa sababu ni njia nzuri ya wanafunzi wangu kufahamiana na wa-Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
No comments:
Post a Comment