Friday, February 24, 2012

Ualimu Kazi Ngumu

Mimi ni mmoja wa walimu ambao tunapenda ualimu. Moyo wangu daima umekuwa kwenye ualimu, na sijawahi kuwazia kubadili mwelekeo.

Walimu wanakumbana na vipingamizi kadhaa, kuanzia sera katika sekta ya elimu, hadi tabia za baadhi ya watoto na wazazi. Namsikitikia mwalimu anayeonekana katika hii katuni. Huenda wizara imeamua kuwa watoto wafundishwe dhana kama istilahi, kutohoa au kifyonzeo kabla ya wakati ufaao. Kila somo lazima liende hatua kwa hatua, kufuatana na umri wa mtoto. Utaratibu huu ukifuatwa, itadhihirika kwamba hakuna somo gumu.
(Namshukuru mchoraji wa katuni hii, ingawa nimeshindwa kumtambua na kumtaja ipasavyo).

2 comments:

Mbele said...

Kuna utafiti ambao sasa umekuwa gumzo hivi karibuni, unaoonyesha jinsi mwalimu bora anavyosababisha maisha bora kwa mwanafunzi. Soma makala hii.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hapa ngoma nzito. Masikini hawa wakianza tu kufahamu dhana nzima ya kifyonzeo, basi tunawachepua tena na kuwasukuma katika Kiingereza ambako hata fununu hawana kabisa.

Basi masikini "wasomi" wetu hawa kwenye Kiswahili hawako na na kwenye Kiingereza hawako. Sera yetu ya lugha ni mojawapo ya sera za ajabu kabisa.

Huo utafiti wa Harvard sijui kama unaweza kuwa ni wa Kilimwengu. Sijausoma lakini tayari najiuliza kama kwanza wamejiuliza sababu zinazomfanya mtu awe Mwalimu Bora. Ningependa waende vijijini kule Shinyanga wakaangalie maisha ya mwalimu halafu tuone kama watafikia hitimisho lile lile. Wakati mwingine hata haiwezekani kuwa Mwalimu Bora !!!

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...