Picha hii ni kumbukumbu ya mambo yalivyokuwa enzi za Mwalimu Nyerere. Viongozi hawakuwa mbali na wananchi. Wote walikuwa wanafahamika kwa jina moja la "ndugu," ambayo ni kielelezo muhimu cha itikadi iliyokuwa inatawala. Hapakuwa na usultani kama ilivyo leo.
Tunapiga ngonjera kuwa sultani aliondolewa Visiwani, wakati usultani unaendelea kushamiri nchini.
5 comments:
erneoutMh!! KAUDO nini? Ingekuwa ni leo hii basi nchi yetu ingekuwa na uchumi mzuri kuliko kutumia mamilioni ya kuwanunulia wabunge magari ya fahari.Na huko DODODMA serikali ingewajengea wabunge apartment za kufikia ili kuokoa hela za nchi.Na hizo posho wangeweza kuwaongezea madaktari mishahara au kama ni posho.
tz biashara, umenikumbusha pale serikali hii ilipoanza kazi. Waziri Mkuu Pinda alituambia kuwa amenunuliwa gari la bei kubwa sana kiasi kwamba hakulipokea. Sijui aliwachukulia hatua gani hao waliolinunua, na sijui kama alipiga marufuku ununuaji wa magari ya aina hii, kwani siamini kama lilikuwa hili moja tu.
Nasikia wenzetu Rwanda walishapiga marufuku magari ya fahari. Nini kinachoizuia serikali ya Tanzania kufanya hivyo hivyo?
Kwanza niseme tu kwamba serikali inatakiwa kupunguza gharama ili tuendane na matatizo ya uchumi kwa kipindi hiki.Wenzetu nchi zilizoendelea wanapunguza na sisi ndio tunautangaza ufahari wakati nchi yenyewe haijaka kaa sawa.
Na kingine nadhani hawa wabunge wakipewa hizi posho kubwa huwa wanapanda kichwa na hawajitumi ipasavyo.Kama watalipwa kidogo basi utaona jinsi watakavo fanya kazi bila ya jeuri.
Hapa Marekani, unaweza kuishi jirani na milionea na usitambue, kwani utamkuta anaishi maisha ya kawaida kabisa. Usishangae kumwona anapita mitaani na baiskeli. Hapa chuoni kwangu, sijawahi kumwona mkuu wa chuo akija ofisini na gari. Anakuja kwa mguu, kwani anakaa kiasi cha robo maili kutoka ofisini. Sisi Bongo, angekuwa na dreva kabisa, wa kumleta na kumrudisha, na kumpeleka nyumbani kula chakula cha mchana. Bongo hata kama kigogo anajua kuendesha gari, kwanza anapewa hilo gari la bei mbaya, halafu anapewa dreva. Kweli Bongo ni kichwa cha mwendawazimu.
Yaani huku uingereza sio tu kuishi na tajiri hata hao viongozi wengine mbona wanadandia treni tena na nauli ni lazima alipe kama hajalipa anashitakiwa.Nakumbuka mke wa Tony Blair wakati ule ni waziri mkuu alipanda treni bila ya kulipa na huezi amini alikamatwa na kulipishwa faini.Huku ndio haki kwa wote hakuna mchezo.
Post a Comment