Friday, January 29, 2021
Africonexion Yashiriki KAN Festival
Shughuli za Africonexion: Cultural Consultants ni kutafiti, kuandika, na kuelimisha kuhusu za tofauti za tamaduni katika dunia ya utandawazi wa leo. Wateja ni wa aina nyingi, kama vile waMarekani wanaokwenda Afrika na waAfrika wanaofika Marekani, taasisi, makampuni, jumuia na vyuo. Lengo ni kuwawezesha watu kuelewa changamoto za tofauti za tamaduni ili kuboresha mahusiano na ufanisi katika shughuli.
Matamasha ni fursa ya kutangaza shughuli za Africonexion: Cultural Consultants, ikiwemo kwa njia ya vitabu na maongezi na watu wanaokuja kwenye meza yetu, na pia ni fursa za kujifunza kutoka kwa watu wanaohudhuria matamasha. Ni fursa za kubadilishana mawazo na uzoefu.
Wednesday, January 27, 2021
Kitabu Kimefika Somalia
Juzi tarehe 25, mama mmoja mSomali aishiye mjini Faribault hapa katika jimbo la Minnesota alinipigia simu. Nilikutana naye mara ya kwanza mwaka jana tamasha la kimataifa Faribault, nikampa nakala ya kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences.
Alivyonipigia jana alisema kuwa alikuwa amerejea kutoka safarini Somalia. Baada ya maongezi na fupi ya simu, aliniandikia ujumbe huu: Joseph, I forgot to tell you that I took your book to Somalia. The people loved reading your book. Yaani, Joseph, nilisahau kukuambia kuwa nilienda na kitabu chako Somalia. Watu walifurahia kusoma kitabu chako.
Nafurahi kuona jinsi kitabu hiki kinavyokubalika na waAfrika wa kila taifa, jinsia, dini, na kadhalika. Kuna vipengele fulani katika kitabu hiki ambavyo ninaposoma, ninapata wasi wasi kuwa huenda niliandika bila kuwaza kuwa kuna waIslamu Afrika. Ajabu ni kuwa waIslamu wenyewe hawajawahi kukwazika. Mmoja kati ya wasomaji wa kitabu hiki wa mwanzo kabisa alikuwa mama muIslamu msomi kutoka Ivory Coast. Alikipenda sana kitabu hiki. WaIslamu wengi wa Afrika, wakiwemo maprofesa wamevutiwa na kitabu hiki. Siku chache zilizopita, nilileta taarifa ya mSomali mwingine. Namshukuru Mungu kwa yote.
Saturday, January 16, 2021
Friday, January 1, 2021
Msomaji Wangu Kutoka Somalia
Huyu ni Salah Habib-Jama Mohamed kutoka Somalia, akiwa na kitabu changu Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Alihitimu shahada ya kwanza hapa katika Chuo cha St. Olaf.
Salah aliniambia katikaa maongezi ya simu kuwa aliwahi kuwa na kitabu hiki akakisoma. Alikipenda sana, ila mtu alikiazima na sasa haijulikani kiko wapi. Nilicheka niliposikia hivyo, kwani nimewasikia waMarekani nao wakilaalamika kuwa nakala zao ziliazimwa na sasa hazijulikani ziliko, kwani waazimaji huwaazimisha wengine, na hivi kitabu kutoweka.
Katika ukurasa wake wa Facebook, Salah aliandika kuhusu kitabu hiki kwamba, "It is a great book and a must read allowing us to understand each other better with humor," yaani ni kitabu bora sana na muhimu kusomwa kwa namna kinavyotuwezesha kuelewana huku kikituchekesha.
Nafurahi kuwa kitabu kinapendwa na wote ambao wamekisoma. Nafarijika kuwa kinapendwa na waAfrika kutoka bara lote, wanawake kwa wanaume, wa makabila na dini mbali mbali. Nafarijika kuwa waMarekank nao wanakipenda, kwani mimi nimeelezea utamaduni wao ingawa si mMarekani. Nashukuru kuwa matokeo yamekuwa hayo.
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...