Friday, October 3, 2008

Mwalimu Julius Nyerere

Nimeona kuwa andiko la kwanza liwe juu ya Mwalimu Julius Nyerere. Mwalimu Nyerere ni mtu maarufu katika historia ya Tanzania. Katika ukumbi huu athari za mawazo na siasa za Mwalimu Nyerere zitajitokeza mara kwa mara, kwani alichangia kuiwezesha Tanzania kupitia hatua ilizopitia, akishirikiana na wazalendo wenzake, ambao nao watakuwa wanatajwa hapa ukumbini, kila itakapobidi.

Mwalimu Nyerere anastahili kukumbukwa, kwa mchango wake mkubwa, sio tu kwa nchi yetu bali kwa dunia. Tunapaswa kusoma maandishi yake na kuyajadili, kuyatathmini, na kuyakarabati inapobidi, ili yaendelee kuwa mwongozo wetu.

Mwalimu Nyerere alikuwa mtu wa fikra, ambaye daima alikuwa anaangalia maslahi ya nchi yetu, na jitihada alizofanya katika kubadilisha siasa, uchumi, utamaduni, na vipengele vingine vya nchi yetu ilikuwa ni kwa nia ya kuikomboa na kuijenga katika misingi ya uhuru, usawa, haki, na kujitegemea. Yako makosa ambayo alifanya, lakini alikuwa mzalendo, aliyeamini kuwa aliyokuwa anafanya ni kwa maslahi ya nchi. Makosa yake yanahitaji kuwekwa katika mkabala huo. Huu ndio mtazamo nitakaokuwa nao katika kuelezea na kujadili mchango wa Mwalimu Nyerere kwa Tanzania na dunia.

3 comments:

Unknown said...

Hongera kwa kumwandika Mwalimu. Yabidi waandishi na wananchi hasa wanafunzi na wasomi tuanze tena kumwongelea... sana... zaidi shauri Afrika na Bongo yahitaji fikra na mfano wake. Mengi yanazidi kuharibika.
Na mimi pia nimemwandika, tazama:
http://www.kitoto.wordpress.com

Anonymous said...

Mbele sikia we kachukue Card Chadema yaani uwe member halafu gombea urais green light 2015.nakwambia mimi.sema uccm wako huo utupilie mbali huko huko.

Mbele said...

Anonymous, mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, wala sijawahi kuwa mwanachama wa CCM. Ukitaka kujua msimamo wangu kuhusu masuala ya demokrasia, vyama vya siasa, na kadhalika, soma kitabu changu cha CHANGAMOTO.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...