Mafisadi Wanaufurahia Mwaka Mpya

Mwaka unaoisha leo, mafisadi wanaoihujumu Tanzania walikuwa na sababu ya kukosa usingizi, kutokana na kampeni kali iliyofanyika dhidi yao.

Ingekuwa vipi, mwaka huu mpya ungekuwa ni mgumu kwa mafisadi, lakini moto uliowashwa dhidi yao umeendelea kuwa hafifu, kwa juhudi za zimamoto. Tumerudi katika amani na utulivu.

Comments

Bro Mbele nakubaliana nawe japo napingana nawe kitu kimoja. Sijui kwa ulivyofumba kama wengi wamekuelewa. Je wasemaje juu ya JK 'kukubali' kiulaini kuandika katiba mpya? Je itakuwa yetu au yao (mafisadi). Hebi tupe uoni wako juu ya hili. Maana jamaa kwa ahadi ni bingwa kama alivyo mahiri wa kutotimiza hata moja zaidi ya sanaa kama kawaida. Heri ya mwaka mpya kwa mara nyingine.Kitabu chako nakalibia kumaliza kukisoma.
Mbele said…
Ndugu Mhango, asante kwa kuupitia ujumbe wangu, na kwa changamoto yako. Ni kweli, nimeweka kama kitendawili, na nategemea watu makini watakitafakari.

Nilianza kuandika kwa jazba fulani, na niliona ninaelekea kuandika makala ndefu. Nilipumzisha akili, nikaamua kuandika kifupi namna hii, kama kitendawili, ambacho kinaweza kusumbua akili katika kukitafakari.

Kama mlivyofanya wanablogu kadhaa tayari, nami niko mbioni kuandika kuhusu hotuba ya JK ya kuukaribisha mwaka mpya. Nitaweka uchambuzi wangu hapa hapa kwenye kijiwe changu.

Wewe ni msomaji makini. Nafurahi kuwa umefika karibu ukingoni katika kusoma hiki kitabu changu, ambacho malengo yake, kama unavyoona kwenye utangulizi, yalikuwa kuchangia maandalizi ya wanafunzi wa ki-Marekani wanaoenda kusoma Afrika. Lakini baada ya hapo, wadau wa sekta na taasisi mbali mbali nao wamekuwa wakikitumia.
Emmanuel said…
Prof. aksante. Nionavyo mimi kama kitendawili nimekipatia vizuri mafisadi wenyewe wameonesha kugawanyika katika suala la katiba. wengine wanasema lazima, wengine hapana, nao baadhi ya viongozi serikali wanapinga wakiongozwa na waziri Kombani na Werema. Ila kwa wengi mafisadi watafurahi kidogo maana wanaona mjadala utakuwa katiba mpya
Christian Bwaya said…
Mafisadi wanajiandaa kufisidi zaidi mwaka huu. Tusubiri tuone au tuchukue hatua? Ah, inategemea.
Mbele said…
Mafisadi walisema kwamba wapinzani wakipewa uongozi wa nchi, amani itavurugika. Ninajiuliza: hivi wapinzani wakipata uongozi, watavuruga amani kwa lengo gani? Sipati jibu, wala sioni mantiki.

Kwa hivi tafsiri inayobaki ni moja, kwamba ni mafisadi ndio wanaowazia kuvuruga amani endapo watapokonywa ulaji.

Popular posts from this blog

Kumbukumbu ya Kuzaliwa

Tenzi Tatu za Kale

Pesa za Majini