Friday, November 9, 2012

U-Islam Watekwa Nyara

Leo nimejipatia kitabu kiitwacho The Great Theft: Wrestling Islam From the Extremists. Mwandishi ni Khaled Abou El Fadl, profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha California, Los Angeles, ambaye kwenye jalada nyuma ya kitabu, ametajwa kuwa "one of the world's preeminent Islamic scholars and an accomplished Islamic jurist."

Nikitafsiri kwa ki-Swahili, ni kwamba mwandishi huyu ni mmoja wa wataalam wa u-Islam ambao wanaongoza hapa duniani na pia ni mwanasheria mahiri wa sheria za ki-Islam. Nimeanza kukisoma kitabu hiki leo hii. Tayari ninaona kuwa hiki kitabu ni moto wa kuotea mbali, kwa jinsi kinavyouelezea na kuutafsiri u-Islam kwa mujibu wa misahafu yake, na kwa jinsi kinavyowabomoa hao wanaoitwa wa-Islam wenye siasa kali. Mwandishi anawabainisha kuwa ni wapotoshaji, kwenye masuala kama nafasi ya wanawake katika u-Islam, jihad, haki za binadamu, ugaidi, na vita.

Kitabu hiki kinanikumbusha kitabu changu kingine, kiitwacho Muhammad: A Biography of the Prophet, ambacho nilikifurahia sana, nikakitaja katika blogu hii. Yeyote anayetaka kujielimisha kuhusu Mtume Muhammad ni vema akasoma kitabu hiki, ambacho gazeti la Muslim News lilikisifu kwamba kinaondoa umbumbumbu uliopo, na ni kitabu muhimu kwa wasio wa-Islam na wa-Islam pia.

Basi nimeona kuwa kitabu cha The Great Theft ni kimoja kati ya hivi vitabu vinavyofafanua kwa umahiri mkubwa ukweli kuhusu u-Islam, tofauti na yale yanayosemwa na hao wanaoitwa wa-Islam wenye siasa kali, ambao wameuteka nyara na wanaupotosha u-Islam. Ushauri wangu ni kuwa tuvisome vitabu hivi. Lakini je, kwa wa-Tanzania, ambao kwwa ujumla ni wavivu wa kujifunza lugha mbali mbali na ni wavivu wa kusoma vitabu, elimu hii itawafikia?

4 comments:

PBF Rungwe Pilot Project said...

Nashukuru Profesa kwa kutumegea habari hizo, na juu ya Kitabu hicho ambacho kama wengi tungelisoma, misuguano iliyopo hapa Tanzania katika ya madhehebu zingepungua kwa kiasi kikubwa. Aidha, changamoto ni kule kutopenda kusoma vitabu, Pengine suluhisho la muda ni kwamba waandishi waweke kazi zao kwenye kwenye midia zingine kama DVD,CD kwa maana walio wengi wanapenda kutazama zaidi kuliko kusoma

Anonymous said...

PBF Rungwe Pilot Project,

I guess that culture was uprooted by the politics of J K Nyerere, Destroying the education all together in Tanzania, and particularly higher education, it was only left and available for the elite.

I guess Professa Mbele before jumping on me on this, DO YOUR HOME WORK. my conviction will tell me that you will come to the same conclusion, ndio maana unastruggle kutoelewa kwanini WATANZANIA WAVIVU WA KUSOMA? Hilo swala nakuachia wewe ulijibu? LIFANYIE KAZI!

kwa ufupi uhalisia wa kusoma ndani ya majumba yetu uliondolewa na kubandikwa usiasa/porojo/umbea/udaku/ubalozi aka ufisadi aka Ujamaa tulioulewa sisi wa Tanzania. Ukiwa na sauti kubwa ndio utapewa idara ya elimu, au kazi kwenye idara yoyote hapa nchini. I know it you know it.. sasa ufanisi utakua wapi.. kwa hiyo culture ya kuongea sana tunayo, and well PERFECTED lakini tukija kwenye kusoma, kuandika ni ZERO..

kwa hiyo madaftari, kazi, and spirit of hard work were thrown out the house..


BUT I AM OTIMISTIC THATS ABOUT TO CHANGE...

my 5 and 6 years old can read and write a short story, know how to use dictionary, and challenge me personally intellectually, and thats the culture we missed in NYERERE DAYS.. what a change..and thats the NEW GENERATION, wakongwe kaeni chonjo...

emuthree said...

Kabla sijaingia kukiosma hicho kitabu, nina mashaka na haya majina, ambayo kiuoni wangu yana kusudio fulani.

Sio kwamba ninakupinga Profesa, hayo uliyosema nayakubali, lakini kuna maneno au majina yametolewa yakiwa na makusudio fulani.

Mimi nilikuwa naomba niambiwe nini maana ya `imani kali' na ili mtu aitwe ana imani kali anakuwa na sifa gani, na hii imani kali ni ya uwongo, na kama ni ya uwongo ni kwa vipi, au ndivyo ilivyo kwenye imani yao! Tusije tukamuhukumu mtu, wakati sisi wenyewe hatuijui imani yake vyema.

Halafu tusichanganye harakati za watu kudai mambo yao, lkn kwa vile hawa watu wana imani hiyo ,basi wao wanaitwa majina ya imani zao, ambayo naona ni tofauti na watu wa imani nyingine. Natumai profesa utanielewa hapo nina maana gani.

Profesa, kuna ule esemi usemao, `ukitaka kumuua mbwa kwanza umuite majiba mbaya' sasa isije ikawa ndilo kusudio la haya majina, sina uhakika na hilo,ndio maana naomba msaada wenu.

Je hawa `waislamu wenye imani kali ni akina nani,na kwanini iwe `waislamu tu...!' isje ikawa ni umagharibi dhidi ya umashariki!

PBF Rungwe Pilot Project said...


Nashukuru Profesa kwa maelezo hayo kuhusu kitabu hi cho.Nami nitakitafuta ili niweze kujua undani wa mambo hayo, maana elimu haina mwisho.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...