Thursday, January 9, 2014

Mdau, Rafiki Yangu

Nina furaha kuongelea habari za huyu bwana tunayeonekana pamoja pichani. Ni mfanyakaxi mwenzangu hapa chuoni St. Olaf. Yeye ni mfanya usafi katika hilo jengo tulimo, lijulikanalo kama Buntrock Commons.

Miezi mingi iliyopita, kabla hatujazoeana, aliniita wakati napita katika jengo hili, akanionyesha nakala ya kitabu changu cha Matengo Folktales, ambacho alikuwa amekinunua. Alionekana mwenye furaha kuwa na kitabu hicho.

Kadiri siku zilvyopita, tukiwa tunaongea, nilipata kufahamu kuwa yeye ni kati ya wale wenye dukuduku na hamu ya kufahamu kuhusu Afrika.

Siku nyingine aliniambia kwa furaha kuwa kijana wake anatarajia kwenda Afrika. Na kweli, miezi ya baadaye aliniambia kijana alishaenda Kenya na Tanzania, akapanda mlima Kilimanjaro.

Katika maongezi yetu ya siku za karibuni, nilimwambia kuwa kwa vile anacho kitabu changu cha Matengo Folktales, nitafurahi kumpa kingine tofauti ambacho nilikichapisha baadaye. Basi, jana tulikutana, nikampa nakala ya Africans and Americans ambayo anaonekana amekishika hapo pichani.


2 comments:

Anonymous said...

Na wewe nawe huna jipya kutaka kutuonesha uko na white men .Mie sijaona point ulotaka kutupa hapa .
umeniotezea muda kusoma story yako.Utadhani unatafita kura za chama fulani

Mbele said...

Andika kuhusu mambo unayoyajua. Karibu watu wote wa chuo hiki ni wazungu, kuanzia wanafunzi, walimu, na wafanya kazi. Nilifika hapa kufundisha mwaka 1991, na kwa miaka yapata 18 mwalimu mw-Afrika nilikuwa mimi tu. Wanafunzi darasani kwangu karibu kila muhula ni wazungu tu.

Nakumbuka kuna mdau mmoja aliona picha wanafunzi wangu na mimi akauliza, Mbona wanafunzi wote ni wazungu tu.

Nawaona ni watu sawa na watu wengine, na hatuna tatizo lolote. Wewe una matatizo. Usilete kasumba zako hapa.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...