Mama Kutoka Togo Kaja Tena Kununua Kitabu

Jana jioni, yule Mama kutoka Togo, ambaye nilimwelezea siku chache zilizopita, alifika tena hapa kwangu, akanunua nakala nyingine ya kitabu cha Africans and Americans. Alisema ni kwa ajili ya marafiki zake, Mark na Carol, wa-Marekani. Aliniomba nisaini, nami nikafanya hivyo.

 Kama kawaida, huwa naandika taarifa za aina hiyo katika blogu hii, tangu zamani. Ni kumbukumbu zangu. 

Nilipata taabu sana kuandika kitabu hiki, ingawa kinaonekana kidogo. Nilihangaika nacho kwa miezi mingi. Miezi sita ya mwisho ya mwaka 2004 nilikuwa katika likizo iitwayo "sabbatical."

Nilitumia fursa hii kushughulikia mswada wangu. Nilikuwa natumia masaa mengi karibu kila siku katika kazi hii. Nafarijika na kufurahi kuona matunda ya jasho langu.

Siku za usoni, Mungu akipenda, nitaelezea taabu nilizopata na mbinu nilizotumia katika kufanikisha uandishi wake.

Comments

Anonymous said…
Naona kama kimedoda. Yaani una mteja mmoja tu! Kitangaze zaidi huenda kikanunuliwa kaka.
Mbele said…
Namtaja mtu ninayemfahamu.Kitabu kimeshanunuliwa sana, na bado kinanunuliwa na watu ambao siwajui, mitandaoni Amazon, lulu.com na kadhalika. Wasomaji wanakitangaza, wala sihitaji kufanya kazi hiyo.

Iila ni uamuzi wangu kuwataja hao wachache, kwa sababu zangu mwenyewe. Nitaendelea kufanya hivyo, kwani habari zao ni kumbukumbu muhimu kwangu.

Mimi ni mpenda vitabu, na vitabu vyangu hadi sasa vinazidi elfu tatu. Ninaongelea vitabu sana, katika blogu hii.

Popular posts from this blog

Kumbukumbu ya Kuzaliwa

Tenzi Tatu za Kale

Pesa za Majini