Nashukuru niliandika kitabu kiitwacho Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Nasema hivi kutokana na jinsi kinavyothaminiwa na watu wanaokitumia. Taarifa hizi ninazipata kutoka kwao.
Wiki hii kwa mfano, nimepata mawasiliano kutoka kwa waalimu wawili. Profesa Artika Tyner, kiongozi mojawapo wa Chuo Kikuu cha St. Thomas ameniandikia kuwa anahitaji nakala za kitabu hii, nami nimempelekea. Niliwahi kumwongelea katika blogu hii, baada ya kukutana naye kwa mara ya kwanza. Tangu tukutane, amekuwa mpiga debe wangu wa dhati. Namshukuru.
Nimepata pia ujumbe kutoka kwa Profesa Barbara Zust wa Chuo cha Gustavus Adolphus kunialika kwenda kuongea na wanafunzi anaowapeleka Tanzania katika programu ambayo imedumu miaka mingi. Kama ilivyo kawaida yake, ananiomba nikaongee na wanafunzi kuhusu masuala yaliyomo katika Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Kama kawaida, watakuwa wameskisoma na wanasubiri fursa ya kuniuliza masuali. Miaka yote nimefurahi kukutana na wanafunzi hao.
Ninafarijika na kushukuru kwamba nilijiingiza katika shughuli hii ya kuwasaidia watu kutafakari na kuelewa tofauti za tamaduni na athari za tofauti hizo, ili kujizatiti kabla na wakati wa kukutana na watu w utamaduni wa kigeni. Nashukuru niliandika kitabu hiki, ambacho kimenirahishia kazi hiyo, na papo hapo ni chachu ya tafakari na mazungumzo ya kuelimisha. Nashukuru kuona kuwa wadau kama hao niliowataja, wenye wadhifa mkubwa katika jamii, wanaona umuhimu wa mchango wangu, nami sitawaangusha.
Tuesday, December 4, 2018
Subscribe to:
Posts (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...